Yohana 6:49 - Swahili Revised Union Version Baba zenu waliila mana jangwani; wakafa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wazee wenu walikula mana kule jangwani, lakini walikufa. Biblia Habari Njema - BHND Wazee wenu walikula mana kule jangwani, lakini walikufa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wazee wenu walikula mana kule jangwani, lakini walikufa. Neno: Bibilia Takatifu Baba zenu walikula mana jangwani, lakini wakafa. Neno: Maandiko Matakatifu Baba zenu walikula mana jangwani, lakini wakafa. BIBLIA KISWAHILI Baba zenu waliila mana jangwani; wakafa. |
Kwa kuwa BWANA alisema juu yao, Hapana budi watakufa nyikani. Napo hapakusalia mtu mmoja miongoni mwao, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni.
Baba zetu waliila mana jangwani kama vile ilivyoandikwa, Aliwapa chakula cha mbinguni ili wale.
Hiki ndicho chakula kishukacho kutoka mbinguni; si kama mababa walivyokula, wakafa; bali akilaye chakula hicho ataishi milele.
Tena napenda kuwakumbusha, ijapokuwa mmekwisha kujua haya yote, ya kwamba Bwana, akiisha kuwaokoa watu katika nchi ya Misri, aliwaangamiza baadaye wale wasioamini.
Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea.