Yohana 5:41 - Swahili Revised Union Version Mimi siupokei utukufu kwa wanadamu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Shabaha yangu si kupata sifa kutoka kwa watu. Biblia Habari Njema - BHND “Shabaha yangu si kupata sifa kutoka kwa watu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Shabaha yangu si kupata sifa kutoka kwa watu. Neno: Bibilia Takatifu “Mimi sikubali kutukuzwa na wanadamu, Neno: Maandiko Matakatifu “Mimi sitafuti kutukuzwa na wanadamu. BIBLIA KISWAHILI Mimi siupokei utukufu kwa wanadamu. |
Si kwamba ninaupokea ushuhuda wa wanadamu; lakini ninasema haya ili ninyi mpate kuokoka.
Mnawezaje kuamini ninyi mnaopokeana utukufu ninyi kwa ninyi, na utukufu ule utokao kwa Mungu aliye wa pekee hamwutafuti?
Kisha Yesu, alipotambua ya kuwa walitaka kuja kumshika ili wamfanye mfalme, akajitenga, akaenda tena mlimani yeye peke yake.
Yeye anenaye kwa nafsi yake tu hutafuta utukufu wake mwenyewe; bali yeye anayetafuta utukufu wake aliyemtuma, huyo ni wa kweli, wala ndani yake hamna udhalimu.
Yesu akajibu, Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu si kitu; anitukuzaye ni Baba yangu, ambaye ninyi mwanena kuwa ni Mungu wenu.
Hatukutafuta utukufu kwa wanadamu, wala kwenu, wala kwa wengine, ingawa tungeweza kuwalemea kama Mitume wa Kristo;
Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake.
Maana alipata heshima na utukufu kutoka kwa Mungu Baba hapo alipoletewa sauti iliyotoka katika utukufu mkuu, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.