Yohana 5:40 - Swahili Revised Union Version Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hata hivyo, nyinyi hamtaki kuja kwangu ili mpate uhai. Biblia Habari Njema - BHND Hata hivyo, nyinyi hamtaki kuja kwangu ili mpate uhai. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hata hivyo, nyinyi hamtaki kuja kwangu ili mpate uhai. Neno: Bibilia Takatifu Lakini mnakataa kuja kwangu ili mpate uzima. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini mnakataa kuja kwangu ili mpate uzima. BIBLIA KISWAHILI Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima. |
BWANA, mkombozi wa Israeli, Mtakatifu wake, amwambia hivi yeye anayedharauliwa na wanadamu; yeye anayechukiwa na taifa hili; yeye aliye mtumishi wao watawalao; Wafalme wataona, watasimama; wakuu nao watasujudu; kwa sababu ya BWANA aliye mwaminifu, Mtakatifu wa Israeli aliyekuchagua.
Basi, nilipokuja, mbona hapakuwa na mtu? Nilipoita, mbona hapakuwa na mtu aliyenijibu? Je! Mkono wangu ni mfupi, hata nisiweze kukomboa? Au je! Mimi sina nguvu za kuponya? Tazama, kwa kukemea kwangu naikausha bahari, mito ya maji naifanya kuwa jangwa; samaki wao wanuka kwa sababu hapana maji, nao wafa kwa kiu.
Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku awakusanyavyo pamoja vifaranga wake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka!
Mwizi huja tu kuiba, kuua na kuharibu; mimi nilikuja ili wawe na uzima, tena wawe nao tele.
Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.
Mnayachunguza maandiko kwa sababu mnadhani kuwa ndani yake ninyi mna uzima wa milele; na maandiko yayo hayo ndiyo yanayonishuhudia.
Mnawezaje kuamini ninyi mnaopokeana utukufu ninyi kwa ninyi, na utukufu ule utokao kwa Mungu aliye wa pekee hamwutafuti?
Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu huyo ndiye aliyetiwa mhuri na Baba, yaani, Mungu.
Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.
Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Roho na Bibi arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.