Sikurudi nyuma kuiacha amri ya midomo yake; Nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu,
Yohana 4:32 - Swahili Revised Union Version Akawaambia, Mimi ninacho chakula msichokijua ninyi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini Yesu akawaambia, “Mimi ninacho chakula msichokijua nyinyi.” Biblia Habari Njema - BHND Lakini Yesu akawaambia, “Mimi ninacho chakula msichokijua nyinyi.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini Yesu akawaambia, “Mimi ninacho chakula msichokijua nyinyi.” Neno: Bibilia Takatifu Lakini yeye akawajibu, “Mimi ninacho chakula ambacho ninyi hamkifahamu.” Neno: Maandiko Matakatifu Lakini yeye akawajibu, “Mimi ninacho chakula ambacho ninyi hamkifahamu.” BIBLIA KISWAHILI Akawaambia, Mimi ninacho chakula msichokijua ninyi. |
Sikurudi nyuma kuiacha amri ya midomo yake; Nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu,
Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono; Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha.
Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki Atawafanya wengi kuwa wenye haki; Naye atayachukua maovu yao.
Maneno yako yalionekana, nami nikayala; na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu, na shangwe ya moyo wangu; maana nimeitwa kwa jina lako, Ee BWANA, Mungu wa majeshi.
Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenituma, nikaimalize kazi yake.
Katika mambo yote nimewaonesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea.
Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea.