Yohana 15:27 - Swahili Revised Union Version Nanyi pia mnashuhudia, kwa kuwa tangu mwanzo mmekuwapo pamoja nami. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nanyi pia mtanishuhudia kwa kuwa mmekuwa nami tangu mwanzo. Biblia Habari Njema - BHND Nanyi pia mtanishuhudia kwa kuwa mmekuwa nami tangu mwanzo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nanyi pia mtanishuhudia kwa kuwa mmekuwa nami tangu mwanzo. Neno: Bibilia Takatifu Ninyi nanyi itawapasa kushuhudia kwa sababu mmekuwa pamoja nami tangu mwanzo. Neno: Maandiko Matakatifu Ninyi nanyi itawapasa kushuhudia kwa sababu mmekuwa pamoja nami tangu mwanzo. BIBLIA KISWAHILI Nanyi pia mnashuhudia, kwa kuwa tangu mwanzo mmekuwapo pamoja nami. |
Naye aliyeona ameshuhudia, na ushuhuda wake ni kweli; naye anajua ya kuwa anasema kweli ili ninyi nanyi mpate kusadiki.
Huyu ndiye yule mwanafunzi ayashuhudiaye haya, na aliyeyaandika haya: nasi twajua ya kuwa ushuhuda wake ni kweli.
Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na kote katika Yudea, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
akaonekana siku nyingi na wale waliopanda naye kutoka Galilaya hadi Yerusalemu, ambao sasa ndio walio mashahidi wake mbele ya watu.
Hata Sila na Timotheo walipoteremka kutoka Makedonia, Paulo akasongwa sana na lile neno, akiwashuhudia Wayahudi ya kwamba Yesu ni Kristo.
Usiku ule Bwana akasimama karibu naye, akasema, Uwe na moyo mkuu; kwa sababu, kama ulivyonishuhudia habari zangu Yerusalemu, imekupasa kunishuhudia vivyo hivyo Rumi nako.
mkamwua yule Mkuu wa uzima, ambaye Mungu amemfufua katika wafu; na sisi tu mashahidi wake.
Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote.
Nawasihi wazee walio kwenu, mimi niliye mzee, mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo, na mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadaye;
Kwa mkono wa Silwano, ndugu mwaminifu kama nijuavyo, nimewaandikia kwa maneno machache, kuonya na kushuhudia ya kuwa hii ndiyo neema ya kweli ya Mungu. Simameni imara katika hiyo.
aliyelishuhudia neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu Kristo, yaani, mambo yote aliyoyaona.
Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nilikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu.