Nimewapenda ninyi, asema BWANA. Lakini ninyi mwasema, Umetupendaje? Je! Esau siye ndugu yake Yakobo? Asema BWANA; ila nimempenda Yakobo;
Yohana 15:12 - Swahili Revised Union Version Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hii ndiyo amri yangu: Pendaneni; pendaneni kama nilivyowapenda nyinyi. Biblia Habari Njema - BHND Hii ndiyo amri yangu: Pendaneni; pendaneni kama nilivyowapenda nyinyi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hii ndiyo amri yangu: pendaneni; pendaneni kama nilivyowapenda nyinyi. Neno: Bibilia Takatifu Amri yangu ndiyo hii: Mpendane kama mimi nilivyowapenda ninyi. Neno: Maandiko Matakatifu Amri yangu ndiyo hii: Mpendane kama mimi nilivyowapenda ninyi. BIBLIA KISWAHILI Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi. |
Nimewapenda ninyi, asema BWANA. Lakini ninyi mwasema, Umetupendaje? Je! Esau siye ndugu yake Yakobo? Asema BWANA; ila nimempenda Yakobo;
mkaende katika upendo, kama Kristo naye alivyowapenda ninyi tena akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu ya manukato.
Bwana na awaongeze na kuwazidisha katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile sisi nasi tulivyo kwenu;
Kuhusu upendano, hamna haja niwaandikie; maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana.
Ndugu, imetupasa kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, kama ilivyo wajibu, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo wa kila mtu kwenu kwa mwenzake umekuwa mwingi.
Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo safi.
Neno la mwisho ni hili; muwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu;
Zaidi ya yote iweni na bidii kubwa katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi.
Na hii ndiyo amri yake, kwamba tuliamini jina la Mwana wake Yesu Kristo, na kupendana sisi kwa sisi, kama alivyotupa amri.
Na sasa mama, nakuomba, si kwamba nakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo, kwamba tupendane.