Maana alishikamana na BWANA, hakuacha kumfuata, bali alizishika amri zake BWANA alizomwamuru Musa.
Yohana 14:15 - Swahili Revised Union Version Mkinipenda, mtazishika amri zangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Mkinipenda mtazishika amri zangu. Biblia Habari Njema - BHND “Mkinipenda mtazishika amri zangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Mkinipenda mtazishika amri zangu. Neno: Bibilia Takatifu “Kama mnanipenda, mtazishika amri zangu. Neno: Maandiko Matakatifu “Kama mnanipenda, mtazishika amri zangu. BIBLIA KISWAHILI Mkinipenda, mtazishika amri zangu. |
Maana alishikamana na BWANA, hakuacha kumfuata, bali alizishika amri zake BWANA alizomwamuru Musa.
Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.
Yesu akawaambia, Kama Mungu angekuwa baba yenu, mngenipenda mimi; kwa maana nilitoka kwa Mungu, nami nimekuja; wala sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye ndiye aliyenituma.
Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutotahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.
Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamumwoni sasa, mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu,
Na huu ndio upendo: tuenende kwa kuzifuata amri zake. Hii ndiyo ile amri, kama mlivyosikia tangu mwanzo kwamba mwenende kwayo.