Na mashamba yatanunuliwa katika nchi hii, mnayoitaja, mkisema, Ni ukiwa, haina mwanadamu wala mnyama; imetiwa katika mikono ya Wakaldayo.
Yohana 13:7 - Swahili Revised Union Version Yesu akajibu, akamwambia, Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu akamjibu, “Huelewi sasa ninachofanya lakini utaelewa baadaye.” Biblia Habari Njema - BHND Yesu akamjibu, “Huelewi sasa ninachofanya lakini utaelewa baadaye.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu akamjibu, “Huelewi sasa ninachofanya lakini utaelewa baadaye.” Neno: Bibilia Takatifu Isa akamjibu, “Hivi sasa hutambui lile ninalofanya, lakini baadaye utaelewa.” Neno: Maandiko Matakatifu Isa akamjibu, “Hivi sasa hutambui lile ninalofanya, lakini baadaye utaelewa.” BIBLIA KISWAHILI Yesu akajibu, akamwambia, Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye. |
Na mashamba yatanunuliwa katika nchi hii, mnayoitaja, mkisema, Ni ukiwa, haina mwanadamu wala mnyama; imetiwa katika mikono ya Wakaldayo.
Nami nikasikia, lakini sikuelewa; ndipo nikasema, Ee Bwana wangu, mwisho wa mambo haya utakuwaje?
Mambo hayo wanafunzi wake hawakuyafahamu hapo kwanza; lakini Yesu alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka ya kwamba ameandikiwa hayo, na ya kwamba walimtendea hayo.
Simoni Petro akamwambia, Bwana, unakwenda wapi? Yesu akamjibu, Niendako huwezi kunifuata sasa; lakini utanifuata baadaye.
Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.