Ndivyo alivyofanya Nuhu, sawasawa na vyote alivyomwamuru Mungu, hivyo ndivyo alivyofanya.
Yohana 13:17 - Swahili Revised Union Version Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, ikiwa mwayajua hayo, mtakuwa na heri mkiyatekeleza. Biblia Habari Njema - BHND Basi, ikiwa mwayajua hayo, mtakuwa na heri mkiyatekeleza. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, ikiwa mwayajua hayo, mtakuwa na heri mkiyatekeleza. Neno: Bibilia Takatifu Sasa kwa kuwa mmejua mambo haya, heri kwenu mkiyatenda. Neno: Maandiko Matakatifu Sasa kwa kuwa mmejua mambo haya, heri yenu ninyi kama mkiyatenda. BIBLIA KISWAHILI Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda. |
Ndivyo alivyofanya Nuhu, sawasawa na vyote alivyomwamuru Mungu, hivyo ndivyo alivyofanya.
Naye BWANA akaniambia, Hubiri maneno haya yote katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu, ukisema, Yasikieni maneno ya maagano haya, mkayafanye.
Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.
Kwa maana yeyote atakayeyafanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye kaka yangu, na dada yangu na mama yangu.
Kwa sababu sio wale waisikiao sheria walio wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale waitendao sheria watakaohesabiwa haki.
Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutotahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.
Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.
Heri wazifuao nguo zao, ili wawe na haki ya kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.