Yohana 11:43 - Swahili Revised Union Version Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alipokwisha sema hayo, akaita kwa sauti kubwa: “Lazaro! Toka nje!” Biblia Habari Njema - BHND Alipokwisha sema hayo, akaita kwa sauti kubwa: “Lazaro! Toka nje!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alipokwisha sema hayo, akaita kwa sauti kubwa: “Lazaro! Toka nje!” Neno: Bibilia Takatifu Baada ya kusema haya, Isa akapaza sauti yake, akaita, “Lazaro, njoo huku!” Neno: Maandiko Matakatifu Baada ya kusema haya, Isa akapaza sauti yake, akaita, “Lazaro, njoo huku!” BIBLIA KISWAHILI Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje. |
Nami nilijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nilisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma.
Akatoka nje yule aliyekufa, akiwa amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.
Basi, siku sita kabla ya Pasaka, Yesu alifika Bethania, alipokuwapo Lazaro, yeye ambaye Yesu alimfufua katika wafu.
Basi watu wengi katika Wayahudi walipata kujua ya kuwa yeye yuko huko, nao wakaja, si kwa ajili yake Yesu tu, ila wamwone na Lazaro, ambaye Yesu alimfufua katika wafu.
Wakati Petro alipoyaona haya akawajibu wale watu, Enyi Waisraeli, mbona mnastaajabia haya, au mbona mnatukazia macho sisi, kana kwamba tumemfanya huyu aende kwa nguvu zetu sisi, au kwa utauwa wetu sisi?
Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende.
Petro akawatoa nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena, Tabitha, inuka. Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi.