Yohana 10:8 - Swahili Revised Union Version Wote walionitangulia ni wezi na wanyang'anyi; lakini kondoo hawakuwasikia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wale wengine wote waliokuja kabla yangu ni wezi na wanyanganyi, nao kondoo hawakuwasikiliza. Biblia Habari Njema - BHND Wale wengine wote waliokuja kabla yangu ni wezi na wanyanganyi, nao kondoo hawakuwasikiliza. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wale wengine wote waliokuja kabla yangu ni wezi na wanyang'anyi, nao kondoo hawakuwasikiliza. Neno: Bibilia Takatifu Wote walionitangulia ni wezi na wanyang’anyi, nao kondoo hawakuwasikia. Neno: Maandiko Matakatifu Wote walionitangulia ni wevi na wanyang’anyi, lakini kondoo hawakuwasikia. BIBLIA KISWAHILI Wote walionitangulia ni wezi na wanyang'anyi; lakini kondoo hawakuwasikia. |
Mwanadamu, toa unabii juu ya wachungaji wa Israeli, toa unabii, uwaambie, naam, hao wachungaji, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wachungaji wa Israeli, wanaojilisha wenyewe; je! Haiwapasi wachungaji kuwalisha kondoo?
Wakuu wake walio ndani yake ni simba wangurumao; mahakimu wake ni mbwamwitu wa jioni; wasiobakiza kitu chochote mpaka asubuhi.
Kwa maana, tazama, mimi nitainua katika nchi hii mchungaji, ambaye hatawaangalia waliopotea, wala hatawatafuta waliotawanyika, wala hatamganga aliyevunjika, wala hatamlisha aliye mzima; bali atakula nyama ya wanono, na kuziraruararua kwato zao.
Yesu aliwaambia, Amin, amin, nawaambieni, Yeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo, lakini akwea penginepo, huyo ni mwizi naye ni mnyang'anyi.
Kwa sababu kabla ya siku hizi aliondoka Theuda, akijidai ya kuwa yeye ni mtu mkuu, watu wapatao mia nne wakashikamana naye; naye aliuawa na wote waliomsadiki wakatawanyika wakawa si kitu.