Yoeli 3:3 - Swahili Revised Union Version Nao wamewapigia kura watu wangu; na mvulana wamemwuza ili kupata kahaba, na msichana wamemwuza ili kupata divai, wapate kunywa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema na kugawana watu wangu kwa kura. Waliwauza wavulana ili kulipia malaya, na wasichana ili kulipia divai. Biblia Habari Njema - BHND na kugawana watu wangu kwa kura. Waliwauza wavulana ili kulipia malaya, na wasichana ili kulipia divai. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza na kugawana watu wangu kwa kura. Waliwauza wavulana ili kulipia malaya, na wasichana ili kulipia divai. Neno: Bibilia Takatifu Waliwapigia kura watu wangu na kuwauza wavulana ili kupata makahaba; waliwauza wasichana ili wapate kunywa mvinyo. Neno: Maandiko Matakatifu Wanawapigia kura watu wangu na kuwauza wavulana ili kupata makahaba; waliwauza wasichana ili wapate kunywa mvinyo. BIBLIA KISWAHILI Nao wamewapigia kura watu wangu; na mvulana wamemwuza ili kupata kahaba, na msichana wamemwuza ili kupata divai, wapate kunywa. |
Ugiriki na Tubali na Mesheki ndio waliokuwa wachuuzi wako; walitoa wanadamu, na vyombo vya shaba, kwa biashara yako.
Levukeni, enyi walevi, mkalie; Pigeni yowe, ninyi nyote mnywao divai; Kwa sababu ya divai mpya; Maana umekatiliwa mbali na vinywa vyenu.
Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Israeli, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wamewauza wenye haki kwa fedha, na maskini kwa jozi ya viatu;
Siku ile uliposimama upande, siku ile wageni walipochukua mali zake, na watu wa kabila nyingine walipoingia katika malango yake, na kumpigia kura Yerusalemu, wewe nawe ulikuwa kama mmoja wao.
Hata hivyo alichukuliwa mbali, alikwenda utumwani; watoto wake wachanga walisetwa kwenye maachano ya njia kuu zote; watu wake wenye heshima wakapigiwa kura, na wakuu wake wote wakafungwa kwa minyororo.
na mdalasini, iliki, uvumba, marhamu, ubani, mvinyo, mafuta ya mzeituni, unga mzuri na ngano, ng'ombe na kondoo, farasi na magari, na miili na roho za wanadamu.