Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Amosi 2:6 - Swahili Revised Union Version

6 Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Israeli, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wamewauza wenye haki kwa fedha, na maskini kwa jozi ya viatu;

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Waisraeli wametenda dhambi tena na tena, kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu. Wamewauza watu waaminifu kwa kuwa hawakuweza kulipa madeni yao; na kuwauza watu fukara wasioweza kulipa deni la kandambili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Waisraeli wametenda dhambi tena na tena, kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu. Wamewauza watu waaminifu kwa kuwa hawakuweza kulipa madeni yao; na kuwauza watu fukara wasioweza kulipa deni la kandambili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Waisraeli wametenda dhambi tena na tena, kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu. Wamewauza watu waaminifu kwa kuwa hawakuweza kulipa madeni yao; na kuwauza watu fukara wasioweza kulipa deni la kandambili.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Kwa dhambi tatu za Israeli, hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. Wanawauza wenye haki kwa fedha, na maskini kwa jozi ya viatu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Hili ndilo asemalo bwana: “Kwa dhambi tatu za Israeli, hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. Wanawauza wenye haki kwa fedha, na maskini kwa jozi ya viatu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

6 Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Israeli, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wamewauza wenye haki kwa fedha, na maskini kwa jozi ya viatu;

Tazama sura Nakili

Amosi 2:6
21 Marejeleo ya Msalaba  

Mfalme wa Ashuru akawahamisha Israeli mpaka Ashuru, akawaweka katika Hala, na katika Habori, karibu na mto wa Gozani, na katika miji ya Wamedi;

kwa sababu hawakuitii sauti ya BWANA, Mungu wao, bali waliyavunja maagano yake, mambo yote ambayo Musa mtumishi wa BWANA aliwaamuru, wasikubali kuyasikiliza, wala kuyatenda.

ili kumpotosha mhitaji asipate haki yake, na kuwanyang'anya maskini wa watu wangu haki yao; ili wajane wawe mateka yao, na kuwafanya yatima waliofiwa na baba zao kuwa mawindo yao!

hao wamfanyao mtu kuwa amekosa katika neno, na kumtegea mtego yeye aonyaye langoni, na kumgeuza mwenye haki kwa kitu kisichofaa.

Basi, tazama, nimeipigia kofi hiyo faida uliyopata kwa njia isiyo haki, na hiyo damu yako iliyokuwa kati yako.

Nao wamewapigia kura watu wangu; na mvulana wamemwuza ili kupata kahaba, na msichana wamemwuza ili kupata divai, wapate kunywa.

tena watoto wa Yuda na watoto wa Yerusalemu mmewauzia Wagiriki, mpate kuwahamisha mbali na nchi yao;

ambalo wenye kundi hilo huwachinja, kisha hujiona kuwa hawana hatia; na hao wawauzao husema, Na ahimidiwe BWANA, kwa maana mimi ni tajiri; na wachungaji wao wenyewe hawawahurumii.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo