Angalia Sayuni, mji wa sikukuu zetu; macho yako yatauona Yerusalemu umekuwa makao ya raha; hema isiyotikisika; vigingi vyake havitang'olewa, wala kamba zake hazitakatika.
Yoeli 3:20 - Swahili Revised Union Version Bali Yuda atadumu milele, na Yerusalemu tangu kizazi hata kizazi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Bali Yuda itakaliwa milele, na Yerusalemu kizazi hata kizazi. Biblia Habari Njema - BHND Bali Yuda itakaliwa milele, na Yerusalemu kizazi hata kizazi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Bali Yuda itakaliwa milele, na Yerusalemu kizazi hata kizazi. Neno: Bibilia Takatifu Yuda itakaliwa na watu milele na Yerusalemu itadumu vizazi vyote. Neno: Maandiko Matakatifu Yuda itakaliwa na watu milele na Yerusalemu itadumu vizazi vyote. BIBLIA KISWAHILI Bali Yuda atadumu milele, na Yerusalemu tangu kizazi hata kizazi. |
Angalia Sayuni, mji wa sikukuu zetu; macho yako yatauona Yerusalemu umekuwa makao ya raha; hema isiyotikisika; vigingi vyake havitang'olewa, wala kamba zake hazitakatika.
Nao watakaa katika nchi niliyompa Yakobo, mtumishi wangu, walimokaa baba zenu; nao watakaa humo, wao na watoto wao, na watoto wa watoto wao, milele; na Daudi, mtumishi wangu, atakuwa mkuu wao milele.
Nami nitawapanda katika nchi yao, wala hawatang'olewa tena watoke katika nchi yao niliyowapa, asema BWANA, Mungu wako.