Mikaya akasema, Sikia basi neno la BWANA; Nilimwona BWANA ameketi katika kiti chake cha enzi, na jeshi lote la mbinguni wamesimama upande wa mkono wake wa kulia na wa kushoto.
Yobu 2:1 - Swahili Revised Union Version Tena ilitukia siku moja hao wana wa Mungu walipokwenda kujiweka mbele za BWANA, Shetani naye akaenda kati yao, ili kujiweka mbele za BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ikatokea tena siku nyingine, malaika wa Mungu walikwenda kukutana mbele ya Mwenyezi-Mungu, naye Shetani akajitokeza pia pamoja nao. Biblia Habari Njema - BHND Ikatokea tena siku nyingine, malaika wa Mungu walikwenda kukutana mbele ya Mwenyezi-Mungu, naye Shetani akajitokeza pia pamoja nao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ikatokea tena siku nyingine, malaika wa Mungu walikwenda kukutana mbele ya Mwenyezi-Mungu, naye Shetani akajitokeza pia pamoja nao. Neno: Bibilia Takatifu Siku nyingine wana wa Mungu walienda kujionesha mbele za Mwenyezi Mungu. Shetani naye akaja pamoja nao kujionesha mbele zake. Neno: Maandiko Matakatifu Siku nyingine wana wa Mungu walikuja kujionyesha mbele za bwana. Shetani naye akaja pamoja nao kujionyesha mbele zake. BIBLIA KISWAHILI Tena ilitukia siku moja hao wana wa Mungu walipokwenda kujiweka mbele za BWANA, Shetani naye akaenda kati yao, ili kujiweka mbele za BWANA. |
Mikaya akasema, Sikia basi neno la BWANA; Nilimwona BWANA ameketi katika kiti chake cha enzi, na jeshi lote la mbinguni wamesimama upande wa mkono wake wa kulia na wa kushoto.
Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujiweka mbele za BWANA, Shetani naye akaenda kati yao.
Kisha BWANA akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu.
BWANA akamwuliza Shetani, Umetoka wapi? Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Natoka katika kuzungukazunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.
Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?
Malaika akamjibu akamwambia, Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele za Mungu; nami nimetumwa niseme nawe, na kukupasha habari hizi njema.
Akasema, Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano;