Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Walawi 13:23 - Swahili Revised Union Version

Lakini ikiwa kipaku hicho king'aacho kimekaa pale pale, wala hakienei, ni kovu ya jipu; na kuhani atasema kwamba yu safi.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Lakini, kama ile sehemu haijaenea, basi, lile ni kovu la jipu tu. Kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa safi.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Lakini, kama ile sehemu haijaenea, basi, lile ni kovu la jipu tu. Kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa safi.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Lakini, kama ile sehemu haijaenea, basi, lile ni kovu la jipu tu. Kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa safi.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Lakini ikiwa ile alama haijabadilika wala kuenea, ni kovu tu kutokana na jipu, kuhani atamtangaza kuwa safi.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Lakini ikiwa ile alama haijabadilika wala kuenea, ni kovu tu kutokana na jipu, kuhani atamtangaza kuwa safi.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Lakini ikiwa kipaku hicho king'aacho kimekaa pale pale, wala hakienei, ni kovu la jipu; na kuhani atasema kwamba yu safi.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Walawi 13:23
13 Marejeleo ya Msalaba  

Yuda akavikiri, akasema, Yeye ni mwenye haki kuliko mimi, kwa kuwa sikumpa Shela, mwanangu. Wala hakumjua tena baada ya hayo.


Daudi akamwambia Nathani, Nimemfanyia BWANA dhambi. Nathani akamwambia Daudi, BWANA naye ameiondoa dhambi yako; hutakufa.


Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.


na kwamba pameenea katika ngozi, ndipo kuhani atasema kwamba ni najisi; hili ni pigo.


Au mwili wa mtu ukiwa una mahali palipoungua katika ngozi yake, kisha pakawa kidonda, kikawa kipaku chekundu kidogo, au cheupe;


Lakini kuhani akipaangalia, nywele nyeupe hamna katika hicho kipaku king'aacho, nacho hakikuingia ndani kuliko ngozi, lakini chafifia; ndipo kuhani atamweka mahali muda wa siku saba;


Petro akalikumbuka lile neno la Yesu alilolisema, Kabla ya jogoo kuwika, utanikana mara tatu. Akatoka nje, akalia kwa majonzi.


hata kinyume cha hayo, ni afadhali mmsamehe na kumfariji, mtu kama huyo asije akamezwa katika huzuni yake ipitayo kiasi.


Ndugu zangu, mtu akishikwa katika kosa lolote, ninyi mlio wa Roho mrejesheni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe.