Wafilipi 2:20 - Swahili Revised Union Version Maana sina mtu mwingine mwenye nia moja nami, atakayeiangalia hali yenu kweli kweli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sina mtu mwingine kama yeye ambaye anawashughulikieni kwa moyo. Biblia Habari Njema - BHND Sina mtu mwingine kama yeye ambaye anawashughulikieni kwa moyo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sina mtu mwingine kama yeye ambaye anawashughulikieni kwa moyo. Neno: Bibilia Takatifu Sina mtu mwingine kama yeye, ambaye ataangalia hali yenu kwa halisi. Neno: Maandiko Matakatifu Sina mtu mwingine kama yeye, ambaye ataangalia hali yenu kwa halisi. BIBLIA KISWAHILI Maana sina mtu mwingine mwenye nia moja nami, atakayeiangalia hali yenu kweli kweli. |
Naye aliyasema hayo, si kwa kuwahurumia maskini; bali kwa kuwa ni mwizi, naye ndiye aliyeshika mfuko, akavichukua vilivyotiwa humo.
Na Mungu mwenye saburi na faraja awajalie kunuia mamoja ninyi kwa ninyi, kwa kufuata mfano wa Kristo Yesu;
Lakini, Timotheo akija, angalieni akae kwenu pasipo hofu; maana anaifanya kazi ya Bwana vile vile kama mimi mwenyewe;
ijalizeni furaha yangu, ili muwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, mkiwaza mamoja.
Ila mwajua sifa yake, ya kuwa ametumika pamoja nami kwa ajili ya Injili, kama mwana na baba yake.
Na Yesu aitwaye Yusto awasalimu. Hao tu ndio watu wa tohara miongoni mwa wale watendao kazi pamoja nami kwa ajili ya ufalme wa Mungu; nao wamekuwa msaada kwangu.
kwa Timotheo, mwanangu halisi katika imani. Na iwe kwako neema, rehema na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.
Uwakumbushe ndugu mambo hayo, nawe utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, na mzoefu wa maneno ya imani, na mafundisho mazuri yale uliyoyafuata.
nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika nyanya yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo.
Bali wewe umeyafuata mafundisho yangu, na mwenendo wangu, na makusudi yangu, na imani, na uvumilivu,
Ikawa Daudi alipokwisha kusema na Sauli, roho ya Yonathani, ikaambatana na roho ya Daudi, Yonathani akampenda kama roho yake mwenyewe.