Musa akatwaa nusu ya ile damu, akaitia katika mabakuli; na nusu ya ile damu akainyunyiza juu ya madhabahu.
Waebrania 9:21 - Swahili Revised Union Version Na ile hema nayo na vyombo vyote vya ibada alivinyunyizia damu vivyo hivyo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Vilevile Mose aliinyunyizia damu ile hema na vyombo vya ibada. Biblia Habari Njema - BHND Vilevile Mose aliinyunyizia damu ile hema na vyombo vya ibada. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Vilevile Mose aliinyunyizia damu ile hema na vyombo vya ibada. Neno: Bibilia Takatifu Vivyo hivyo alinyunyizia damu hiyo kwenye ile hema pamoja na kila kifaa kilichotumika ndani yake kwa taratibu za ibada. Neno: Maandiko Matakatifu Vivyo hivyo alinyunyizia damu hiyo kwenye ile hema pamoja na kila kifaa kilichotumika ndani yake kwa taratibu za ibada. BIBLIA KISWAHILI Na ile hema nayo na vyombo vyote vya ibada alivinyunyizia damu vivyo hivyo. |
Musa akatwaa nusu ya ile damu, akaitia katika mabakuli; na nusu ya ile damu akainyunyiza juu ya madhabahu.
Kisha twaa baadhi ya damu ya ng'ombe, uitie katika pembe za madhabahu kwa kidole chako; na kuimimina damu yote chini ya madhabahu.
Kisha utamchinja kondoo, na kuitwaa damu yake, na kuitia katika ncha ya sikio la Haruni la upande wa kulia, na katika ncha za masikio ya kulia ya wanawe, na katika vyanda vya gumba vya mikono yao ya kulia, na katika vidole vikuu vya miguu yao ya kulia, na kuinyunyiza hiyo damu katika madhabahu kuizunguka kandokando.
Kila siku utamtoa ng'ombe dume wa sadaka ya dhambi kwa ajili ya upatanisho; nawe utaisafisha hiyo madhabahu, hapo utakapofanya upatanisho kwa ajili ya hiyo madhabahu; nawe utaitia mafuta, ili kuitakasa.
Kisha utayatwaa mafuta ya kutiwa, na kuitia mafuta hiyo maskani, na kila kitu kilicho ndani yake, na kuiweka iwe takatifu, na vyombo vyake vyote; nayo itakuwa takatifu.
Kisha akamchinja; na Musa akaitwaa damu yake, akaitia katika pembe za madhabahu pande zote kwa kidole chake, akaitakasa madhabahu, kisha akaimwaga hiyo damu hapo chini ya madhabahu, na kuitakasa, ili afanye upatanisho kwa ajili yake.
Huyo ng'ombe dume naye akamchinja, na huyo kondoo dume pia, dhabihu ya sadaka za amani, zilizokuwa kwa ajili ya watu; na wanawe Haruni wakamsogezea ile damu, naye akainyunyiza katika madhabahu pande zote,