Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Waebrania 7:5 - Swahili Revised Union Version

Na katika wana wa Lawi nao, wale waupatao ukuhani, wana amri kutwaa sehemu ya kumi kwa watu wao, yaani, ndugu zao, kwa agizo la sheria, ijapokuwa wametoka katika uzao wa Abrahamu.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Tunajua pia kwamba kufuatana na sheria, wazawa wa Lawi ambao ni makuhani, wanayo haki ya kuchukua sehemu moja ya kumi kutoka kwa watu, yaani ndugu zao, ingawaje nao ni wazawa wa Abrahamu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Tunajua pia kwamba kufuatana na sheria, wazawa wa Lawi ambao ni makuhani, wanayo haki ya kuchukua sehemu moja ya kumi kutoka kwa watu, yaani ndugu zao, ingawaje nao ni wazawa wa Abrahamu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Tunajua pia kwamba kufuatana na sheria, wazawa wa Lawi ambao ni makuhani, wanayo haki ya kuchukua sehemu moja ya kumi kutoka kwa watu, yaani ndugu zao, ingawaje nao ni wazawa wa Abrahamu.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Basi sheria inawaagiza wana wa Lawi ambao hufanyika makuhani kupokea sehemu ya kumi kutoka kwa watu ambao ni ndugu zao, ingawa ndugu zao ni wazao wa Ibrahimu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Basi sheria inawaagiza wana wa Lawi ambao hufanyika makuhani kupokea sehemu ya kumi kutoka kwa watu ambao ni ndugu zao, ingawa ndugu zao ni wazao wa Ibrahimu.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Na katika wana wa Lawi nao, wale waupatao ukuhani, wana amri kutwaa sehemu ya kumi kwa watu wao, yaani, ndugu zao, kwa agizo la sheria, ijapokuwa wametoka katika uzao wa Abrahamu.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Waebrania 7:5
15 Marejeleo ya Msalaba  

Mungu akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uzidi ukaongezeke. Taifa na kundi la mataifa watatoka kwako, na wafalme watatoka katika uzao wako.

Watu wote waliokuja pamoja na Yakobo mpaka Misri, waliokuwa wazawa wake, bila wake za wanawe, walikuwa watu sitini na sita.

Lakini wewe hutanijengea nyumba hiyo; ila mwanao utakayemzaa wewe mwenyewe, yeye ndiye atakayeijenga nyumba kwa jina langu.

Tena nikagundua kwamba Walawi hawakupewa sehemu zao; Hivyo Walawi na waimbaji walioongoza ibada, kila mtu amerudi shambani mwake.

Na wale watu wote waliotokana na uzao wa Yakobo walikuwa watu sabini; na huyo Yusufu alikuwa huko ndani ya Misri tangu hapo.

Nawe umlete Haruni ndugu yako karibu nami, na wanawe pamoja naye, miongoni mwa wana wa Israeli, ili anitumikie katika kazi ya ukuhani. Haruni, na Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari, wana wa Haruni.

Nawe na wanao pamoja nawe mtautunza ukuhani wenu, kwa ajili ya kila kitu cha madhabahu, na kwa ajili ya vile vilivyomo ndani ya pazia, nanyi mtatumika. Nawapeni ukuhani kuwa utumishi wa kipawa; na mgeni akaribiaye atauawa.

Utakapokwisha kutoa zaka, katika zaka zote za mavuno yako mwaka wa tatu, ambao ndio mwaka wa kutolea zaka, umpe zile zaka Mlawi, na mgeni, na yatima, na mjane, wapate kula ndani ya malango yako na kushiba;

Na hapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii, ila yeye aitwaye na Mungu, kama vile Haruni.

kwa maana alikuwa katika viuno vya baba yake, hapo Melkizedeki alipokutana naye.