Waebrania 2:7 - Swahili Revised Union Version Umemfanya mdogo kwa muda kuliko malaika, Umemvika taji la utukufu na heshima, Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ulimfanya tu kidogo kuwa chini ya malaika; umemvika taji ya utukufu na heshima, Biblia Habari Njema - BHND Ulimfanya tu kidogo kuwa chini ya malaika; umemvika taji ya utukufu na heshima, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ulimfanya tu kidogo kuwa chini ya malaika; umemvika taji ya utukufu na heshima, Neno: Bibilia Takatifu Umemfanya chini kidogo kuliko malaika; ukamvika taji la utukufu na heshima, Neno: Maandiko Matakatifu Umemfanya chini kidogo kuliko malaika; ukamvika taji ya utukufu na heshima, BIBLIA KISWAHILI Umemfanya mdogo punde kuliko malaika, Umemvika taji la utukufu na heshima, Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; |
bali utukufu na heshima na amani kwa kila mtu atendaye mema, Myahudi kwanza na Mgiriki pia;
wale ambao kwa subira katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutoharibika, watapewa uzima wa milele;
Sasa kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu peke yake, na iwe heshima na utukufu milele na milele. Amina.
ila twamwona yeye aliyefanywa mdogo kwa muda kuliko malaika, yaani, Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji la utukufu na heshima, ili kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya kila mtu.