Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Waebrania 2:6 - Swahili Revised Union Version

6 Mwanadamu ni nini hata umkumbuke, Ama mwana wa binadamu, hata umwangalie?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Tena yasemwa mahali fulani katika Maandiko: “Mtu ni nini, hata umfikirie; mwanadamu ni nini hata umjali?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Tena yasemwa mahali fulani katika Maandiko: “Mtu ni nini, hata umfikirie; mwanadamu ni nini hata umjali?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Tena yasemwa mahali fulani katika Maandiko: “Mtu ni nini, hata umfikirie; mwanadamu ni nini hata umjali?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Lakini kuna mahali mtu mmoja ameshuhudia, akisema: “Mwanadamu ni kitu gani hata unamfikiria, binadamu ni nani hata unamjali?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Lakini kuna mahali mtu fulani ameshuhudia akisema: “Mwanadamu ni kitu gani hata unamfikiria, binadamu ni nani hata unamjali?

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

6 Mwanadamu ni nini hata umkumbuke, Ama mwana wa binadamu, hata umwangalie?

Tazama sura Nakili




Waebrania 2:6
16 Marejeleo ya Msalaba  

Yusufu akawaambia ndugu zake, Mimi ninakufa, lakini Mungu atawajia ninyi bila shaka, atawapandisha toka nchi hii, mpaka nchi aliyowaapia Abrahamu, na Isaka, na Yakobo.


Je! Mwanadamu ni kitu gani, hata akawa safi? Huyo aliyezaliwa na mwanamke, hata awe na haki?


Seuze mtu, aliye mdudu! Na mwanadamu, ambaye ni buu!


Ee BWANA, mtu ni kitu gani hata umjali? Na binadamu hata umwangalie?


Mataifa yote huwa kama si kitu mbele zake; huhesabiwa kwake kuwa duni kabisa na batili.


Mimi, naam, mimi, ndimi niwafarijiye; wewe u nani hata ukamwogopa mtu atakayekufa, na mwanadamu atakayefanywa kuwa kama majani?


Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, Kwa kuwa amewajia watu wake, na kuwakomboa.


Kwa njia ya rehema za Mungu wetu, Ambazo kwa hizo mwangaza utokao juu umetufikia,


Hofu ikawashika wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Nabii mkuu ametokea kwetu; na, Mungu amewaangalia watu wake.


Mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosea katika jambo hili; kwa sababu Bwana ndiye alipizaye kisasi cha haya yote; kama tulivyowaambia kwanza, tukashuhudia sana.


Kwa maana ameinena siku ya saba mahali fulani hivi, Mungu alistarehe siku ya saba, akaziacha kazi zake zote;


Kama asemavyo mahali pengine, Ndiwe kuhani milele Kwa mfano wa Melkizedeki.


Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo