Ondokeni, mwende zenu; maana hapa sipo mahali pa raha yenu; kwa sababu ya uchafu mtaangamizwa, naam, kwa maangamizo makubwa sana.
Waebrania 13:14 - Swahili Revised Union Version Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana hapa duniani hatuna mji wa kudumu; lakini tunautafuta ule unaokuja. Biblia Habari Njema - BHND Maana hapa duniani hatuna mji wa kudumu; lakini tunautafuta ule unaokuja. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana hapa duniani hatuna mji wa kudumu; lakini tunautafuta ule unaokuja. Neno: Bibilia Takatifu Kwa kuwa hapa hatuna mji udumuo, bali tunautafuta ule ujao. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa kuwa hapa hatuna mji udumuo, bali tunautafuta ule ujao. BIBLIA KISWAHILI Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao. |
Ondokeni, mwende zenu; maana hapa sipo mahali pa raha yenu; kwa sababu ya uchafu mtaangamizwa, naam, kwa maangamizo makubwa sana.
Lakini, ndugu, nasema hivi, muda ubakio si mwingi; basi tokea sasa wale walio na wake na wawe kama hawana;
Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda mfupi tu, yatuandalia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana;
Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu.
Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo;
Maana mliwaonea huruma wale waliokuwa katika vifungo, tena mkakubali kwa furaha kunyang'anywa mali zenu, mkijua kwamba nafsini mwenu mna mali iliyo njema zaidi, idumuyo.
Bali ninyi mmeufikia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,
Lakini neno lile, Mara moja tena, ladhihirisha kuhamishwa vile viwezavyo kutetemeshwa, kama vitu vilivyoumbwa, vitu visivyoweza kutetemeshwa vikae.
Maana hakuuweka chini ya malaika ulimwengu ule ujao tunaounena, ila mtu mmoja ameshuhudia hivi mahali fulani, akisema,
Lakini Kristo akiisha kuja, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo, kwa hema iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu,
Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya.