Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Ufunuo 3:12 - Swahili Revised Union Version

12 Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 “Mshindi nitamfanya awe nguzo katika hekalu la Mungu wangu, na hatatoka humo kamwe. Pia nitaandika juu yake jina la Mungu wangu na jina la mji wa Mungu wangu, yaani Yerusalemu mpya, mji ambao utashuka kutoka juu mbinguni kwa Mungu wangu. Tena nitaandika juu yake jina langu jipya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 “Mshindi nitamfanya awe nguzo katika hekalu la Mungu wangu, na hatatoka humo kamwe. Pia nitaandika juu yake jina la Mungu wangu na jina la mji wa Mungu wangu, yaani Yerusalemu mpya, mji ambao utashuka kutoka juu mbinguni kwa Mungu wangu. Tena nitaandika juu yake jina langu jipya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 “Mshindi nitamfanya awe nguzo katika hekalu la Mungu wangu, na hatatoka humo kamwe. Pia nitaandika juu yake jina la Mungu wangu na jina la mji wa Mungu wangu, yaani Yerusalemu mpya, mji ambao utashuka kutoka juu mbinguni kwa Mungu wangu. Tena nitaandika juu yake jina langu jipya.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Yeye ashindaye nitamfanya kuwa nguzo katika Hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo kamwe. Nitaandika juu yake Jina la Mungu wangu na jina la mji mkubwa wa Mungu wangu, Yerusalemu mpya, ambao unashuka kutoka mbinguni kwa Mungu wangu. Nami pia nitaandika juu yake Jina langu jipya.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Yeye ashindaye nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo kamwe. Nitaandika juu yake Jina la Mungu wangu na jina la mji mkubwa wa Mungu wangu, Yerusalemu mpya, ambao unashuka kutoka mbinguni kwa Mungu wangu. Nami pia nitaandika juu yake Jina langu jipya.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

12 Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 3:12
26 Marejeleo ya Msalaba  

Akazisimamisha nguzo ukumbini pa hekalu; akaisimamisha nguzo ya kulia, akaiita jina lake Yakini; akaisimamisha nguzo ya kushoto, akaiita jina lake Boazi.


Kuna mto, vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu, Patakatifu pa maskani zake Aliye Juu.


Kama tulivyosikia, ndivyo tulivyoona, Katika mji wa BWANA wa majeshi. Mji wa Mungu wetu; Mungu atauimarisha hata milele.


Mambo makuu yanasemwa kukuhusu, Ee Mji wa Mungu.


Na mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha BWANA.


Nanyi mtaliacha jina lenu kuwa laana kwa wateule wangu. Na Bwana MUNGU atakuua; naye atawaita watumishi wake kwa jina lingine.


Maana, tazama, nimekufanya leo kuwa mji wenye boma, na nguzo ya chuma, na kuta za shaba, juu ya nchi yote; juu ya wafalme wa Yuda, na juu ya wakuu wake, na juu ya makuhani wake, na juu ya watu wa nchi hii.


Urefu wa ukumbi ulikuwa dhiraa ishirini, na upana wake dhiraa kumi na moja; karibu na madaraja ambayo waliupandia; tena palikuwa na nguzo karibu na miimo, moja upande huu, na moja upande huu.


Kuuzunguka ni mianzi elfu kumi na nane; na jina la mji huo tangu siku hiyo litakuwa hili, BWANA yupo.


Wakaileta. Akawaambia, Ni ya nani sanamu hii na anwani hii? Wakamwambia, Ni ya Kaisari.


tena Yakobo, Kefa, na Yohana, waliosifika kuwa ni nguzo, walipoitambua ile neema niliyopewa, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kulia wa kuonesha ushirikiano; ili sisi tuende kwa Mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara;


ambaye kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa,


Bali ninyi mmeufikia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,


Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao.


Ninyi, watoto wadogo, mnatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia.


Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu elfu mia moja na arubaini na nne pamoja naye, wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.


Hawa watafanya vita na Mwana-kondoo, na Mwana-kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu.


Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.


Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea.


Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.


Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.


nao watamwona uso wake, na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao.


Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo