Waebrania 12:12 - Swahili Revised Union Version Kwa hiyo inyosheni mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, inueni mikono yenu inayolegea na kuimarisha magoti yenu yaliyo dhaifu. Biblia Habari Njema - BHND Basi, inueni mikono yenu inayolegea na kuimarisha magoti yenu yaliyo dhaifu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, inueni mikono yenu inayolegea na kuimarisha magoti yenu yaliyo dhaifu. Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo, itieni nguvu mikono yenu iliyo dhaifu na magoti yenu yaliyolegea. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo, itieni nguvu mikono yenu iliyo dhaifu na magoti yenu yaliyolegea. BIBLIA KISWAHILI Kwa hiyo inyosheni mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza, |
Na itakuwa, wakuambiapo, Mbona unapiga kite? Ndipo utakaposema, Kwa sababu ya habari hizo, maana linakuja; na kila moyo utayeyuka, na mikono yote itakuwa dhaifu, na kila roho itazimia, na magoti yote yatageuka kuwa kama maji; tazama, linakuja, nalo litatendeka, asema Bwana MUNGU.
Ndipo uso wa mfalme ukambadilika; fikira zake zikamfadhaisha; viungo vya viuno vyake vikalegea; magoti yake yakagongana.
Amekuwa utupu, na ukiwa, na uharibifu; hata moyo unayeyuka, na magoti yanagonganagongana; moyoni kote mna uchungu, na nyuso za wote zimekuwa nyeupe kwa hofu.
Ndugu, tunawasihi, waonyeni wale wasiokaa kwa utaratibu; watieni moyo walio dhaifu; watieni nguvu wanyonge; vumilieni na watu wote.
Maana mtafakarini sana yeye aliyeyastahimili upinzani mkuu namna hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu.
tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau maonyo ya Bwana, Wala usife moyo ukiadhibiwa naye;