Waebrania 10:31 - Swahili Revised Union Version Ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kuanguka mikononi mwa Mungu aliye hai ni jambo la kutisha mno! Biblia Habari Njema - BHND Kuanguka mikononi mwa Mungu aliye hai ni jambo la kutisha mno! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kuanguka mikononi mwa Mungu aliye hai ni jambo la kutisha mno! Neno: Bibilia Takatifu Ni jambo la kutisha kuanguka mikononi mwa Mungu aliye hai. Neno: Maandiko Matakatifu Ni jambo la kutisha kuanguka mikononi mwa Mungu aliye hai. BIBLIA KISWAHILI Ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai. |
Katika siku hiyo Misri itakuwa kama wanawake; itatetemeka na kuogopa kwa sababu ya kutikiswa kwa mkono wa BWANA wa majeshi, autikisao juu yake.
Wenye dhambi walio katika Sayuni wanaogopa; tetemeko limewashika wasiomcha Mungu; Ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uangamizao; ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uteketezao milele?
Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika Jehanamu.
Lakini nitawaonya mtakayemwogopa; mwogopeni yule ambaye akiisha kumwua mtu ana uweza wa kumtupa katika Jehanamu; naam, nawaambia, Mwogopeni huyo.
kutakuwa na mitetemeko mikubwa ya ardhi; na njaa na tauni mahali pengi; na mambo ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni.
Basi, angalia, mkono wa Bwana uko juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazungukazunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza.
Basi tukiijua hofu ya Bwana, twawavuta wanadamu; lakini tumedhihirishwa mbele za Mungu. Nami natumaini ya kuwa tumedhihirishwa katika dhamiri zenu pia.
bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.
Hadharini, ndugu zangu, usiwepo katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutoamini, ujitengao na Mungu aliye hai.