nawe utakuwa heri, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa; kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.
Ufunuo 20:5 - Swahili Revised Union Version Hao wafu waliobakia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema (Wale wengine waliokufa hawakupata uhai mpaka miaka 1,000 itimie). Huu ndio ufufuo wa kwanza. Biblia Habari Njema - BHND (Wale wengine waliokufa hawakupata uhai mpaka miaka 1,000 itimie). Huu ndio ufufuo wa kwanza. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza (Wale wengine waliokufa hawakupata uhai mpaka miaka 1,000 itimie). Huu ndio ufufuo wa kwanza. Neno: Bibilia Takatifu (Wafu waliosalia hawakufufuka hadi ilipotimia hiyo miaka elfu.) Huu ndio ufufuo wa kwanza. Neno: Maandiko Matakatifu (Wafu waliosalia hawakufufuka mpaka ilipotimia hiyo miaka 1,000.) Huu ndio ufufuo wa kwanza. BIBLIA KISWAHILI Hao wafu waliobakia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu. |
nawe utakuwa heri, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa; kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.
Maana ikiwa kutupwa kwao kumeleta upatanisho kwa ulimwengu, je! Kukubaliwa kwao kutakuwa nini kama si uhai baada ya kufa?
Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
Na baada ya siku hizo tatu u nusu, roho ya uhai itokayo kwa Mungu ikawaingia, wakasimama kwa miguu yao; na hofu kuu ikawaangukia watu waliowatazama.
Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele.