Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Ufunuo 11:7 - Swahili Revised Union Version

Hata watakapoumaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika kuzimu atafanya vita nao, naye atawashinda na kuwaua.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Lakini wakisha maliza kutoa unabii huo, mnyama atokaye shimoni kuzimu atapigana nao, atawashinda na kuwaua.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Lakini wakisha maliza kutoa unabii huo, mnyama atokaye shimoni kuzimu atapigana nao, atawashinda na kuwaua.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Lakini wakisha maliza kutoa unabii huo, mnyama atokaye shimoni kuzimu atapigana nao, atawashinda na kuwaua.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Basi watakapokuwa wamemaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika lile Shimo atapigana nao vita, atawashinda na kuwaua.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Basi watakapokuwa wamemaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika lile Shimo atapigana nao vita, atawashinda na kuwaua.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Hata watakapoumaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye kuzimu atafanya vita nao, naye atawashinda na kuwaua.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Ufunuo 11:7
20 Marejeleo ya Msalaba  

Naye atanena maneno kinyume chake Aliye Juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye Juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa nyakati tatu na nusu


Akawaambia, Nendeni, mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilisha kazi yangu.


Wakamsihi asiwaamuru watoke kwenda shimoni.


Mimi nimekutukuza duniani, nikiwa nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.


Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema, Imekwisha. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake.


Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na huduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Habari Njema ya neema ya Mungu.


Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;


Nami nitawaruhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini, wakiwa wamevikwa magunia.


Joka likamkasirikia yule mwanamke, likaenda zake lifanye vita juu ya wazawa wake waliobakia, wanaozishika amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; nalo likasimama juu ya mchanga wa bahari.


Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili kama Mwana-kondoo, akanena kama joka.


Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa.