Sefania 2:2 - Swahili Revised Union Version kabla haijatolewa hiyo amri, kabla siku ile haijapita kama makapi, kabla haijawajia hasira kali ya BWANA, kabla haijawajia siku ya hasira ya BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema kabla hamjapeperushwa mbali kama makapi, kabla haijawajia siku ya hasira kali ya Mwenyezi-Mungu, kabla haijawajia siku ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND kabla hamjapeperushwa mbali kama makapi, kabla haijawajia siku ya hasira kali ya Mwenyezi-Mungu, kabla haijawajia siku ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza kabla hamjapeperushwa mbali kama makapi, kabla haijawajia siku ya hasira kali ya Mwenyezi-Mungu, kabla haijawajia siku ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu kabla wakati ulioamriwa haujafika na siku ile inayopeperusha kama makapi, kabla hasira kali ya Mwenyezi Mungu haijaja juu yenu, kabla siku ya ghadhabu ya Mwenyezi Mungu haijaja juu yenu. Neno: Maandiko Matakatifu kabla ya wakati ulioamriwa haujafika na siku ile inayopeperusha kama makapi, kabla hasira kali ya bwana haijaja juu yenu, kabla siku ya ghadhabu ya bwana haijaja juu yenu. BIBLIA KISWAHILI kabla haijatolewa hiyo amri, kabla siku ile haijapita kama makapi, kabla haijawajia hasira kali ya BWANA, kabla haijawajia siku ya hasira ya BWANA. |
Shikeni yaliyo bora, asije akafanya hasira Nanyi mkapotea njiani, Kwa kuwa hasira yake huwaka upesi; Heri wote wanaomkimbilia.
Mataifa wananguruma kama ngurumo ya maji mengi; Lakini atawakemea, nao watakimbia mbali sana, Watafukuzwa kama makapi milimani mbele ya upepo, Na kama mavumbi vuruvuru mbele ya tufani.
Hasira ya BWANA haitarudi, hata atakapokwisha kuyatimiza makusudi ya moyo wake; katika siku za mwisho mtalifahamu neno hili kabisa.
Jitahirini kwa BWANA, mkayaondoe magovi ya mioyo yenu, enyi watu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu; ghadhabu yangu isije ikatoka kama moto, ikawaka hata mtu asiweze kuizima, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu.
BWANA ameitimiza ghadhabu yake, Ameimimina hasira yake kali; Naye amewasha moto katika Sayuni Ulioiteketeza misingi yake.
Maana mimi ni BWANA; mimi nitanena, na neno lile nitakalolinena litatimizwa; wala halitakawilishwa tena; maana katika siku zenu, Ewe nyumba iliyoasi, nitalinena neno hilo na kulitimiza, asema Bwana MUNGU.
Kwa sababu hiyo watakuwa kama wingu la asubuhi, na kama umande utowekao upesi, kama makapi yaliyopeperushwa na tufani sakafuni, na kama moshi utokao katika bomba.
Ni nani awezaye kusimama mbele za ghadhabu yake, naye ni nani awezaye kukaa katika ukali wa hasira yake? Hasira yake kali humwagwa kama moto, nayo majabali yapasuliwa na yeye.
Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya BWANA; bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, mwisho wa kutisha.
Basi ningojeeni, asema BWANA, hata siku ile nitakapoondoka kuteka mateka; maana nimeazimia kuwakusanya mataifa, ili nizikutanishe falme, nipate kuwamwagia ghadhabu yangu; naam, ukali wote wa hasira yangu; kwa maana dunia yote itateketezwa kwa moto wa wivu wangu.