Yuda wakakusanyika pamoja ili wamtafute BWANA; hata kutoka miji yote ya Yuda wakaja kumtafuta BWANA.
Sefania 2:1 - Swahili Revised Union Version Jikusanyeni, naam, jikusanyeni, Ee taifa lisilo na haya; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kusanyikeni, kusanyikeni enyi taifa la watu wasio na aibu, Biblia Habari Njema - BHND Kusanyikeni, kusanyikeni enyi taifa la watu wasio na aibu, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kusanyikeni, kusanyikeni enyi taifa la watu wasio na aibu, Neno: Bibilia Takatifu Kusanyikeni pamoja, kusanyikeni pamoja, enyi taifa lisilo na aibu, Neno: Maandiko Matakatifu Kusanyikeni pamoja, kusanyikeni pamoja, enyi taifa lisilo na aibu, BIBLIA KISWAHILI Jikusanyeni, naam, jikusanyeni, Ee taifa lisilo na haya; |
Yuda wakakusanyika pamoja ili wamtafute BWANA; hata kutoka miji yote ya Yuda wakaja kumtafuta BWANA.
Na watu wote wakakusanyika kama mtu mmoja katika uwanja uliokuwa mbele ya lango la maji; wakamwambia Ezra, mwandishi, akilete kitabu cha Torati ya Musa, BWANA aliyowaamuru Israeli.
Hata siku ya ishirini na nne ya mwezi huo wana wa Israeli wakawa wamekusanyika, wakifunga, wenye kuvaa magunia, na kujitia udongo vichwani.
Nenda ukawakusanye Wayahudi wote waliopo hapa Susa, mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kisha nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie.
Kwa sababu hiyo manyunyu yamezuiliwa, wala hapakuwa na mvua ya vuli; hata hivyo ulikuwa na kipaji cha uso cha kahaba, ulikataa kutahayarika.
Je! Walitahayarika, walipokuwa wameunda machukizo? La, hawakutahayarika hata kidogo, wala hawakuweza kuona haya usoni; basi, wataanguka miongoni mwa hao waangukao; wakati nitakapowajia wataangushwa chini, asema BWANA.
Takaseni saumu, iteni kusanyiko la dini, Wazee na wakusanye wenyeji wote wa nchi; Waende nyumbani kwa BWANA, Mungu wenu, Na kumlilia BWANA,
BWANA kati yake ni mwenye haki; hatatenda uovu; kila asubuhi hudhihirisha hukumu yake, wala hakomi; bali mtu asiye haki hajui kuona haya.
Nami nikawakatilia mbali wachungaji watatu katika mwezi mmoja; maana nafsi yangu ilikuwa imechoka kwa ajili yao, na nafsi zao pia walinichukia.
Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.