Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Ruthu 1:8 - Swahili Revised Union Version

Kisha Naomi akawaambia wakweze wawili, Nendeni sasa mkarejee kila mmoja nyumbani kwa mamaye; BWANA na awatendee mema ninyi, kama ninyi mlivyowatendea mema hao waliofariki na mimi pia.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Naye Naomi akawaambia hao wakwe zake wawili, “Rudini kila mmoja nyumbani kwa mama yake. Naomba Mwenyezi-Mungu awe mwema kwenu kama mlivyokuwa wema kwangu na kwa wale watu wangu waliofariki.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Naye Naomi akawaambia hao wakwe zake wawili, “Rudini kila mmoja nyumbani kwa mama yake. Naomba Mwenyezi-Mungu awe mwema kwenu kama mlivyokuwa wema kwangu na kwa wale watu wangu waliofariki.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Naye Naomi akawaambia hao wakwe zake wawili, “Rudini kila mmoja nyumbani kwa mama yake. Naomba Mwenyezi-Mungu awe mwema kwenu kama mlivyokuwa wema kwangu na kwa wale watu wangu waliofariki.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Ndipo Naomi akawaambia wale wakwe wake wawili, “Rudini, kila mmoja wenu nyumbani mwa mama yake. Mwenyezi Mungu na awatendee mema kama mlivyowatendea hao waliofariki, na mimi pia.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Ndipo Naomi akawaambia wale wakwe zake wawili, “Rudini, kila mmoja wenu nyumbani kwa mama yake. bwana na awatendee fadhili kama mlivyowatendea hao waliofariki, na pia mimi.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Kisha Naomi akawaambia wakweze wawili, Nendeni sasa mkarejee kila mmoja nyumbani kwa mamaye; BWANA na awatendee mema ninyi, kama ninyi mlivyowatendea mema hao waliofariki na mimi pia.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Ruthu 1:8
14 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA naye sasa awatendee ninyi fadhili na kweli; mimi nami nitawalipeni fadhili hiyo, kwa sababu mmetenda jambo hilo.

Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu.

Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana.

mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Kristo.

wote wawili Maloni na Kilioni wakafa; na huyo mwanamke akawa amefiwa na wanawe wawili, na mumewe pia.

Basi akatoka pale alipokuwa akiishi, na wakweze wawili pamoja naye; wakashika njia ili kurudi mpaka nchi ya Yuda.

BWANA na awajalie kuona raha kila mmoja nyumbani kwa mumewe. Kisha akawabusu; nao wakapaza sauti zao wakalia.

Naye Naomi akamwambia mkwewe, Na abarikiwe huyo na BWANA, ambaye hakuuacha wema wake, wala kwa hao walio hai wala kwa waliokufa. Kisha Naomi akamwambia, Mtu huyu ni wa ukoo wetu, mmojawapo wa jamaa yetu aliye karibu.

Akamwambia, Mwanangu, ubarikiwe na BWANA; umezidi kuonesha fadhili zako mwisho kuliko mwanzo, kwa vile usivyowafuata vijana, wawe ni maskini au matajiri.