Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Ruthu 1:5 - Swahili Revised Union Version

5 wote wawili Maloni na Kilioni wakafa; na huyo mwanamke akawa amefiwa na wanawe wawili, na mumewe pia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Mahloni na Kilioni nao pia walifariki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Mahloni na Kilioni nao pia walifariki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Mahloni na Kilioni nao pia walifariki.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Maloni na Kilioni pia wakafa. Basi Naomi akabaki hana mume wala wanawe wawili.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Maloni na Kilioni pia wakafa. Basi Naomi akabaki hana mume wala wanawe wawili.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

5 wote wawili Maloni na Kilioni wakafa; na huyo mwanamke akawa amefiwa na wanawe wawili, na mumewe pia.

Tazama sura Nakili




Ruthu 1:5
9 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo utasema moyoni mwako, Ni nani aliyenizalia watoto hawa, na mimi nimefiwa na watoto wangu, nami niko peke yangu, nimehamishwa, ninatangatanga huko na huku? Tena ni nani aliyewalea hawa? Tazama, niliachwa peke yangu; hawa je! Walikuwa wapi?


Uovu wako mwenyewe utakurudi, maasi yako yatakukaripia; ujue, basi, ukaone, ya kuwa ni jambo baya sana na uchungu, kuwa umemwacha BWANA, Mungu wako, na ya kuwa moyoni mwako hamna kunihofu, asema Bwana, BWANA wa majeshi.


Na alipolikaribia lango la mji, hapo palikuwa na maiti anachukuliwa nje, ni mwana pekee wa mamaye ambaye ni mjane, na watu wengi mjini walikuwa pamoja naye.


Fahamu sasa ya kuwa Mimi, naam, Mimi ndiye, Wala hapana Mungu mwingine ila Mimi; Naua Mimi, nahuisha Mimi, Nimejeruhi, tena naponya; Wala hapana awezaye kuokoa katika mkono wangu,


Na jina la mtu huyo aliitwa Elimeleki, na jina la mkewe Naomi, na majina ya wanawe wawili Maloni na Kilioni, Waefrata wa Bethlehemu ya Yuda. Wakafika nchi ya Moabu, wakakaa huko.


Nao wakaoa wanawake wa Kimoabu, jina la mmoja aliitwa Orpa, na jina la wa pili Ruthu. Baada ya kukakaa huko miaka kumi hivi,


Ndipo alipoondoka, yeye na wakweze, ili kurudi kutoka nchi ya Moabu; maana akiwa katika nchi ya Moabu alipata habari kuwa BWANA alikuwa amewajia watu wake na kuwapa chakula.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo