Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Obadia 1:1 - Swahili Revised Union Version

Maono yake Obadia. Ndivyo asemavyo Bwana MUNGU juu ya Edomu; Tumepata habari kwa BWANA, Na mjumbe ametumwa kati ya mataifa, Akisema, Haya, inukeni ninyi; Na tuinuke tupigane naye.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Maono ya Obadia. Mambo aliyosema Bwana Mwenyezi-Mungu kuhusu taifa la Edomu. Tumepata habari kutoka kwa Mwenyezi-Mungu; mjumbe ametumwa kati ya mataifa: “Inukeni! Twende tukapigane na Edomu!”

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Maono ya Obadia. Mambo aliyosema Bwana Mwenyezi-Mungu kuhusu taifa la Edomu. Tumepata habari kutoka kwa Mwenyezi-Mungu; mjumbe ametumwa kati ya mataifa: “Inukeni! Twende tukapigane na Edomu!”

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Maono ya Obadia. Mambo aliyosema Bwana Mwenyezi-Mungu kuhusu taifa la Edomu. Tumepata habari kutoka kwa Mwenyezi-Mungu; mjumbe ametumwa kati ya mataifa: “Inukeni! Twende tukapigane na Edomu!”

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Maono ya Obadia. Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi kuhusu Edomu: Tumesikia ujumbe kutoka kwa Mwenyezi Mungu: Mjumbe alitumwa kwa mataifa kusema, “Inukeni, twendeni tukapigane vita dhidi yake.”

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Maono ya Obadia. Hili ndilo asemalo bwana Mwenyezi kuhusu Edomu: Tumesikia ujumbe kutoka kwa bwana: Mjumbe alitumwa kwa mataifa kusema, “Inukeni, twendeni tukapigane vita dhidi yake.”

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Maono yake Obadia. Ndivyo asemavyo Bwana MUNGU juu ya Edomu; Tumepata habari kwa BWANA, Na mjumbe ametumwa kati ya mataifa, Akisema, Haya, inukeni ninyi; Na tuinuke tupigane naye.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Obadia 1:1
28 Marejeleo ya Msalaba  

Esau akamwambia Yakobo, Tafadhali, unipe hicho chakula chekundu nile, kwa kuwa ninazimia mimi. Kwa hiyo walimwita jina lake Edomu.

Esau akakaa katika mlima Seiri, Esau ndiye Edomu.

Hivi ni vizazi vya Esau, baba ya Edomu katika mlima Seiri.

Ee BWANA, uwakumbuke wana wa Edomu, Siku ile Yerusalemu ilipotekwa. Kwa namna walivyosema, Bomoeni! Bomoeni hata misingini!

Ufunuo juu ya Duma. Mtu ananililia toka Seiri, Ee mlinzi, habari gani za usiku? Ee mlinzi, habari gani za usiku?

Mlinzi akasema, Mchana unakuja na usiku pia; mkitaka kuuliza, ulizeni; njoni tena.

Kwa maana wakuu wake wako Soani, na wajumbe wake wamefika Hanesi.

Ndipo nikakipokea kikombe kile mkononi mwa BWANA, nikawanywesha mataifa yote, ambao BWANA alinituma kwao;

Edomu, na Moabu, na wana wa Amoni;

Wala isizimie mioyo yenu, wala msiiogope habari itakayosikiwa katika nchi; maana habari itakuja mwaka mmoja, na baadaye mwaka wa pili habari itakuja, na udhalimu katika nchi, mwenye kutawala akishindana na mwenye kutawala.

Tena neno la BWANA likanijia, kusema,

Misri itakuwa ukiwa, na Edomu itakuwa jangwa tupu, kwa sababu ya dhuluma waliowatenda wana wa Yuda; kwa sababu wamemwaga damu isiyo na hatia katika nchi yao.

Avunjaye amekwea juu mbele yao; Wamebomoa mahali, wakapita mpaka langoni, Wakatoka nje huko; Mfalme wao naye amepita akiwatangulia, Naye BWANA ametangulia mbele yao.

Nanyi mtasikia habari za vita na tetesi za vita; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado.

Nanyi mtakaposikia habari za vita na uvumi wa vita, msitishwe; hayo hayana budi kutukia, lakini ule mwisho bado.