Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 21:11 - Swahili Revised Union Version

11 Ufunuo juu ya Duma. Mtu ananililia toka Seiri, Ee mlinzi, habari gani za usiku? Ee mlinzi, habari gani za usiku?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Kauli ya Mungu dhidi ya Duma. Ninasikia mtu ananiita kutoka Seiri: “Mlinzi, nini kipya leo usiku? Kuna kipya chochote leo usiku?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Kauli ya Mungu dhidi ya Duma. Ninasikia mtu ananiita kutoka Seiri: “Mlinzi, nini kipya leo usiku? Kuna kipya chochote leo usiku?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Kauli ya Mungu dhidi ya Duma. Ninasikia mtu ananiita kutoka Seiri: “Mlinzi, nini kipya leo usiku? Kuna kipya chochote leo usiku?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Neno la unabii kuhusu Duma: Mtu fulani ananiita kutoka Seiri, “Mlinzi, usiku utaisha lini? Mlinzi, usiku utaisha lini?”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Neno kuhusu Duma: Mtu fulani ananiita kutoka Seiri, “Mlinzi, usiku utaisha lini? Mlinzi, usiku utaisha lini?”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

11 Ufunuo juu ya Duma. Mtu ananililia toka Seiri, Ee mlinzi, habari gani za usiku? Ee mlinzi, habari gani za usiku?

Tazama sura Nakili




Isaya 21:11
24 Marejeleo ya Msalaba  

na Mishma, na Duma, na Masa,


Basi, Yakobo akapeleka wajumbe mbele yake kwenda kwa Esau nduguye mpaka nchi ya Seiri katika nyika ya Edomu.


Akawaagiza akisema, Mwambieni hivi bwana wangu, Esau, Hivi ndivyo asemavyo mtumwa wako, Yakobo; Nimekaa ugenini kwa Labani, na kukawia huko hata sasa,


na Mishma, na Duma, na Masa, na Hadadi, na Tema;


Ee BWANA, uwakumbuke wana wa Edomu, Siku ile Yerusalemu ilipotekwa. Kwa namna walivyosema, Bomoeni! Bomoeni hata misingini!


Walinzi wazungukao mjini waliniona; Je! Mmemwona mpendwa wa nafsi yangu?


Mlinzi akasema, Mchana unakuja na usiku pia; mkitaka kuuliza, ulizeni; njoni tena.


Maana Bwana ameniambia hivi, Nenda, weka mlinzi; aonayo na ayatangaze.


ndipo Sedekia, mfalme, akatuma watu wamlete; naye mfalme akamwuliza kwa siri ndani ya nyumba yake, akasema, Je! Liko neno lililotoka kwa BWANA? Yeremia akasema, Liko. Akasema pia, Utatiwa katika mikono ya mfalme wa Babeli.


Nami niliweka walinzi juu yenu, wakisema, Isikilizeni sauti ya tarumbeta; lakini walisema, Hatutaki kusikiliza.


Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa Edomu wametenda kinyume cha nyumba ya Yuda, kwa kujilipiza kisasi, nao wamekosa sana, na kujilipiza kisasi juu yao;


Basi wewe, mwanadamu, nimekuweka kuwa mlinzi kwa nyumba ya Israeli; basi ulisikie neno hili kinywani mwangu, ukawape maonyo yangu.


Misri itakuwa ukiwa, na Edomu itakuwa jangwa tupu, kwa sababu ya dhuluma waliowatenda wana wa Yuda; kwa sababu wamemwaga damu isiyo na hatia katika nchi yao.


Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Gaza, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu waiiteka nyara kabila nzima, wawatie katika mikono ya Edomu;


Na Edomu itakuwa milki Seiri pia itakuwa milki, waliokuwa adui zake; Israeli watakapotenda kwa ushujaa.


msipigane nao; kwa kuwa sitawapa sehemu ya nchi yao kamwe, hata kiasi cha kukanyaga wayo wa mguu; kwa kuwa nimempa Esau milima ya Seiri kuwa milki yake.


Arabu, Duma, Eshani;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo