Akatoka ndugu yake baadaye, ana uzi mwekundu mkononi mwake; naye akaitwa jina lake Zera.
Nehemia 11:24 - Swahili Revised Union Version Na Pethahia, mwana wa Meshezabeli, wa wana wa Zera, mwana wa Yuda, alikuwa wakili wa mfalme kwa habari ya mambo yote ya watu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Pethahia, mwana wa Meshezabeli, wa ukoo wa Zera katika kabila la Yuda, alikuwa mwakilishi kwa mfalme kuhusu mambo yote ya watu wa Yuda. Biblia Habari Njema - BHND Pethahia, mwana wa Meshezabeli, wa ukoo wa Zera katika kabila la Yuda, alikuwa mwakilishi kwa mfalme kuhusu mambo yote ya watu wa Yuda. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Pethahia, mwana wa Meshezabeli, wa ukoo wa Zera katika kabila la Yuda, alikuwa mwakilishi kwa mfalme kuhusu mambo yote ya watu wa Yuda. Neno: Bibilia Takatifu Pethahia mwana wa Meshezabeli, mmoja wa wazao wa Zera mwana wa Yuda, alikuwa mwakilishi wa mfalme katika mambo yote kuhusu mahusiano na watu. Neno: Maandiko Matakatifu Pethahia mwana wa Meshezabeli, mmoja wa wazao wa Zera mwana wa Yuda, alikuwa mwakilishi wa mfalme katika mambo yote kuhusu mahusiano na watu. BIBLIA KISWAHILI Na Pethahia, mwana wa Meshezabeli, wa wana wa Zera, mwana wa Yuda, alikuwa wakili wa mfalme kwa habari ya mambo yote ya watu. |
Akatoka ndugu yake baadaye, ana uzi mwekundu mkononi mwake; naye akaitwa jina lake Zera.
Na wana wa Yuda; Eri, na Onani, na Shela, na Peresi, na Zera; lakini Eri na Onani walikufa katika nchi ya Kanaani. Na wana wa Peresi, ni Hesroni, na Hamuli.
na Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa mkuu wa Wakerethi na Wapelethi; na wana wa Daudi walikuwa mofisa wakuu wa mfalme.
Kwani kazi yao ilikuwa kuwangojea wana wa Haruni katika utumishi wa nyumba ya BWANA, nyuani, na vyumbani, na kwa kuvisafisha vitakatifu vyote, ndiyo kazi ya utumishi wa nyumba ya Mungu;
Na baada yao akaijenga Meremothi, mwana wa Uria, mwana wa Hakosi. Na baada yao akafanyiza Meshulamu, mwana wa Berekia, mwana wa Meshezabeli. Na baada yao akafanyiza Sadoki, mwana wa Baana.
Na wana wa Yuda kwa jamaa zao; wa Shela, jamaa ya Washela; wa Peresi, jamaa ya Waperesi; wa Zera, jamaa ya Wazera.