Msiitumainie dhuluma, Wala msijivune kwa unyang'anyi; Mali izidipo msiiangalie sana moyoni.
Nahumu 3:1 - Swahili Revised Union Version Ole wake mji wa damu! Umejaa mambo ya uongo na unyang'anyi; mateka hayaondoki. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ole wako mji wa mauaji! Umejaa udanganyifu mtupu na nyara tele, usiokoma kamwe kuteka nyara. Biblia Habari Njema - BHND Ole wako mji wa mauaji! Umejaa udanganyifu mtupu na nyara tele, usiokoma kamwe kuteka nyara. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ole wako mji wa mauaji! Umejaa udanganyifu mtupu na nyara tele, usiokoma kamwe kuteka nyara. Neno: Bibilia Takatifu Ole wa mji unaomwaga damu, uliojaa uongo, uliojaa nyara, na usiokosa mateka. Neno: Maandiko Matakatifu Ole wa mji umwagao damu, uliojaa uongo, umejaa nyara, usiokosa kuwa na vitu vya kuteka nyara. BIBLIA KISWAHILI Ole wake mji wa damu! Umejaa mambo ya uongo na unyang'anyi; mateka hayaondoki. |
Msiitumainie dhuluma, Wala msijivune kwa unyang'anyi; Mali izidipo msiiangalie sana moyoni.
Wakati wa jioni, tazama, kuna hofu; Na kabla ya mapambazuko hawako; Hilo ndilo fungu lao watutekao, Na ajali yao wanaotunyang'anya mali zetu.
Ni nani aliyemtoa Yakobo awe mateka, aliyemtia Israeli katika mikono ya wanyang'anyi? Si yeye, BWANA? Yeye tuliyemkosea, ambaye hawakutaka kwenda katika njia zake, wala hawakuitii sheria yake.
Hapana neno ila kuapa kwa uongo, na kuvunja ahadi, na kuua, na kuiba, na kuzini; huruka mpaka, na kumwaga damu mfululizo.
Simba alirarua vipande vipande chakula cha kuwatosha watoto wake, aliwakamatia majike wake mawindo, aliyajaza mapango yake mateka, na makao yake aliyajaza nyama iliyoraruliwa.
Tazama, mimi ni juu yako, asema BWANA wa majeshi, nami nitayateketeza magari yako ya vita katika moshi, na upanga utawaangamiza wanasimba wako; nami nitayakatilia mbali mawindo yako katika nchi, na sauti za wajumbe wako hazitasikiwa tena kamwe.