Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Mwanzo 7:5 - Swahili Revised Union Version

Nuhu akafanya kama vile BWANA alivyomwamuru.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Noa akafanya yote kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Noa akafanya yote kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Noa akafanya yote kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Nuhu akafanya yote Mwenyezi Mungu aliyomwamuru.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Nuhu akafanya yote kama bwana alivyomwamuru.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Nuhu akafanya kama vile BWANA alivyomwamuru.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Mwanzo 7:5
14 Marejeleo ya Msalaba  

Ndivyo alivyofanya Nuhu, sawasawa na vyote alivyomwamuru Mungu, hivyo ndivyo alivyofanya.


Na walioingia, waliingia wa kike na wa kiume, wa kila kitu chenye mwili, kama vile alivyomwamuru Mungu; BWANA akamfungia.


Ndipo mimi sitaaibika, Nikiyaangalia maagizo yako yote.


Basi ndivyo ilivyomalizwa kazi yote ya maskani ya hema ya kukutania; na wana wa Israeli walifanya kama yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyofanya.


Musa akafanya hayo yote; kama BWANA aliyoagiza ndivyo alivyofanya yote.


Musa na Haruni wakafanya vivyo hivyo; kama BWANA alivyowaambia, ndivyo walivyofanya.


Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Ndipo akakubali.


Akawajibu akasema, Mama yangu na ndugu zangu ni hao walisikiao neno la Mungu na kulifanya.


Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda.


Mamaye akawaambia watumishi, Lolote atakalowaambia, fanyeni.


tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.


na, ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata;