Waliingia katika safina alimokuwa Nuhu, wawili wawili, wa kila chenye mwili kilicho na pumzi ya uhai ndani yake.
Mwanzo 7:16 - Swahili Revised Union Version Na walioingia, waliingia wa kike na wa kiume, wa kila kitu chenye mwili, kama vile alivyomwamuru Mungu; BWANA akamfungia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kila aina yao waliingia, dume na jike, kama Mungu alivyomwamuru Noa. Kisha, Mwenyezi-Mungu akaufunga mlango wa safina nyuma yake Noa. Biblia Habari Njema - BHND Kila aina yao waliingia, dume na jike, kama Mungu alivyomwamuru Noa. Kisha, Mwenyezi-Mungu akaufunga mlango wa safina nyuma yake Noa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kila aina yao waliingia, dume na jike, kama Mungu alivyomwamuru Noa. Kisha, Mwenyezi-Mungu akaufunga mlango wa safina nyuma yake Noa. Neno: Bibilia Takatifu Wanyama walioingia katika safina walikuwa wa kiume na wa kike, wa kila kiumbe chenye uhai kama Mungu alivyomwamuru Nuhu; ndipo Mwenyezi Mungu akamfungia ndani. Neno: Maandiko Matakatifu Wanyama walioingia katika safina walikuwa wa kiume na wa kike, wa kila kiumbe chenye uhai kama Mungu alivyomwamuru Nuhu, ndipo bwana akamfungia ndani. BIBLIA KISWAHILI Na walioingia, waliingia wa kike na wa kiume, wa kila kitu chenye mwili, kama vile alivyomwamuru Mungu; BWANA akamfungia. |
Waliingia katika safina alimokuwa Nuhu, wawili wawili, wa kila chenye mwili kilicho na pumzi ya uhai ndani yake.
Ile gharika ilikuwako juu ya nchi siku arubaini; nayo maji yakazidi, yakaifanya safina ielee, ikaelea juu ya nchi.
wakaingia katika safina alimo Nuhu, wawili wawili, wa kike na wa kiume, kama vile Mungu alivyomwamuru Nuhu.
Tazama, yuavunja, wala haiwezekani kujenga tena; Humfunga mtu, wala haiwezekani kumfungua.
Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa.
Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;
Mungu wa milele ndiye makazi yako, Na mikono ya milele i chini yako. Na mbele yako amemsukumia mbali adui; Akasema, Angamiza.
Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani ili mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.