Abrahamu akamtwaa Ishmaeli mwanawe, na wote waliozaliwa nyumbani mwake, na wote walionunuliwa kwa fedha yake, wanaume wote wa watu wa nyumba ya Abrahamu, akawatahiri nyama ya magovi yao siku ile ile, kama Mungu alivyomwambia.
Mwanzo 6:22 - Swahili Revised Union Version Ndivyo alivyofanya Nuhu, sawasawa na vyote alivyomwamuru Mungu, hivyo ndivyo alivyofanya. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Noa akafanya yote kama Mungu alivyomwamuru. Biblia Habari Njema - BHND Noa akafanya yote kama Mungu alivyomwamuru. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Noa akafanya yote kama Mungu alivyomwamuru. Neno: Bibilia Takatifu Nuhu akafanya kila kitu kama vile Mungu alimwamuru. Neno: Maandiko Matakatifu Nuhu akafanya kila kitu kama vile Mungu alivyomwamuru. BIBLIA KISWAHILI Ndivyo alivyofanya Nuhu, sawasawa na vyote alivyomwamuru Mungu, hivyo ndivyo alivyofanya. |
Abrahamu akamtwaa Ishmaeli mwanawe, na wote waliozaliwa nyumbani mwake, na wote walionunuliwa kwa fedha yake, wanaume wote wa watu wa nyumba ya Abrahamu, akawatahiri nyama ya magovi yao siku ile ile, kama Mungu alivyomwambia.
Na walioingia, waliingia wa kike na wa kiume, wa kila kitu chenye mwili, kama vile alivyomwamuru Mungu; BWANA akamfungia.
wakaingia katika safina alimo Nuhu, wawili wawili, wa kike na wa kiume, kama vile Mungu alivyomwamuru Nuhu.
Akaitanda hema juu ya maskani, akakitia kifuniko cha hema juu yake; kama BWANA alivyomwamuru Musa.
kisha akalileta sanduku akalitia ndani ya maskani, naye akalitundika pazia la sitara, akalisitiri sanduku la ushuhuda; kama BWANA alivyomwamuru Musa.
hapo walipoingia hema ya kukutania, na hapo walipoikaribia madhabahu walinawa kama BWANA alivyomwamuru Musa.