Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Mwanzo 50:1 - Swahili Revised Union Version

Yusufu akamwangukia babaye usoni, akamlilila, akambusu.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Hapo Yosefu akamkumbatia baba yake akilia na kumbusu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Hapo Yosefu akamkumbatia baba yake akilia na kumbusu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Hapo Yosefu akamkumbatia baba yake akilia na kumbusu.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Basi Yusufu akamwangukia baba yake, akalilia juu yake na akambusu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Basi Yusufu akamwangukia baba yake, akalilia juu yake na akambusu.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Yusufu akamwangukia babaye usoni, akamlilia, akambusu.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Mwanzo 50:1
11 Marejeleo ya Msalaba  

Sara akafa katika Kiriath-arba, ndio Hebroni, katika nchi ya Kanaani. Abrahamu akamlilia na kumwombolezea Sara.


Mimi nitashuka pamoja nawe mpaka Misri; nami nitakupandisha tena bila shaka; na Yusufu ataweka mkono wake juu ya macho yako.


Basi Yakobo alipokwisha kuwaagiza wanawe, akakunja miguu yake kitandani, akafa, akakusanywa pamoja na watu wake.


Yusufu akawaagiza watumishi wake waganga wampake baba yake dawa asioze. Waganga wakampaka dawa Israeli.


Basi Elisha alikuwa ameshikwa na ugonjwa wake uliomwua; naye Yehoashi mfalme wa Israeli akateremka amtazame, akamlilia mbele yake, akasema, Baba yangu! Baba yangu! Gari la Israeli na wapanda farasi wake!


Watu watauwa wakamzika Stefano, wakamfanyia maombolezo makuu.


Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maagizo ya Bwana.


Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.