Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye Juu Sana, Muumba mbingu na nchi.
Mwanzo 47:10 - Swahili Revised Union Version Yakobo akambariki Farao, akatoka mbele ya Farao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha Yakobo akambariki Farao, akaondoka. Biblia Habari Njema - BHND Kisha Yakobo akambariki Farao, akaondoka. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha Yakobo akambariki Farao, akaondoka. Neno: Bibilia Takatifu Yakobo akambariki Farao, kisha akaondoka mbele yake. Neno: Maandiko Matakatifu Kisha Yakobo akambariki Farao, naye akaondoka mbele ya uso wake. BIBLIA KISWAHILI Yakobo akambariki Farao, akatoka mbele ya Farao. |
Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye Juu Sana, Muumba mbingu na nchi.
Yusufu akawakalisha babaye na nduguze, na kuwapa milki katika nchi ya Misri, katika mahali pazuri pa nchi, katika nchi ya Ramesesi, kama Farao alivyoamuru.
Basi watu wote wakavuka Yordani, naye mfalme akavuka; kisha mfalme akambusu Barzilai, akambariki; naye akarudi nyumbani kwake.
Tou akamtuma Yoramu mwanawe kwa mfalme Daudi ili kumsalimia, na kumpongeza, na kumbariki, kwa sababu amepigana na Hadadezeri, na kumpiga; kwa maana Hadadezeri alikuwa amepigana vita juu ya Tou. Na mkononi mwake Yorabu akaleta vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na vyombo vya shaba;
Hii ndiyo baraka ya Musa, huyo mtu wa Mungu, aliyowabarikia wana wa Israeli kabla ya kufa kwake.
Na tazama, Boazi akaja kutoka Bethlehemu na kuwaamkia wavunaji, akasema, BWANA akae nanyi. Nao wakamwitikia, BWANA na akubariki.