Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 47:11 - Swahili Revised Union Version

11 Yusufu akawakalisha babaye na nduguze, na kuwapa milki katika nchi ya Misri, katika mahali pazuri pa nchi, katika nchi ya Ramesesi, kama Farao alivyoamuru.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Basi, Yosefu akawapa baba yake na ndugu zake eneo la Ramesesi lililo bora kabisa katika nchi ya Misri, liwe makao yao, nao wakalimiliki kama alivyoagiza Farao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Basi, Yosefu akawapa baba yake na ndugu zake eneo la Ramesesi lililo bora kabisa katika nchi ya Misri, liwe makao yao, nao wakalimiliki kama alivyoagiza Farao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Basi, Yosefu akawapa baba yake na ndugu zake eneo la Ramesesi lililo bora kabisa katika nchi ya Misri, liwe makao yao, nao wakalimiliki kama alivyoagiza Farao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Ndipo Yusufu akawakalisha baba yake na ndugu zake katika nchi ya Misri, akawapa milki katika sehemu bora sana ya nchi, ile wilaya ya Ramesesi, kama Farao alivyoelekeza.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Ndipo Yusufu akawakalisha baba yake na ndugu zake katika nchi ya Misri na kuwapa milki katika sehemu bora sana ya nchi, wilaya ya Ramesesi, kama Farao alivyoelekeza.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

11 Yusufu akawakalisha babaye na nduguze, na kuwapa milki katika nchi ya Misri, katika mahali pazuri pa nchi, katika nchi ya Ramesesi, kama Farao alivyoamuru.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 47:11
13 Marejeleo ya Msalaba  

Semeni, Watumishi wako tumekuwa wachunga wanyama tangu ujana wetu, na hata leo, sisi, na baba zetu; mpate kukaa katika nchi ya Gosheni; maana kila mchunga wanyama ni chukizo kwa Wamisri.


Israeli akakaa katika nchi ya Misri, katika nchi ya Gosheni. Wakapata mali humo, wakaongezeka na kuzidi sana.


nchi ya Misri iko mbele yako, palipo pema pa nchi uwakalishe baba yako na ndugu zako; na wakae katika nchi ya Gosheni. Tena ukijua ya kuwa wako watu hodari miongoni mwao, uwaweke wawe wakuu wa wanyama wangu.


Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi.


Wana wa Israeli wakasafiri kutoka Ramesesi mpaka Sukothi, walipata hesabu yao kama watu elfu mia sita wanaume waliokwenda kwa miguu, bila kuhesabu watoto.


Nao wataangika juu yake utukufu wote wa nyumba ya baba yake; wazao wake na watoto wao, kila chombo kidogo tangu vyombo vya vikombe hata vyombo vya makopo vyote pia.


Wakasafiri kutoka Ramesesi mwezi wa kwanza, siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza; siku ya pili baada ya Pasaka, wana wa Israeli wakatoka kwa uhodari mkubwa mbele ya macho ya Wamisri wote,


Mwizi huja tu kuiba, kuua na kuharibu; mimi nilikuja ili wawe na uzima, tena wawe nao tele.


Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu.


Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.


Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.


kama vile ulivyompa mamlaka juu ya watu wote, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele.


Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami popote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo