Mwanzo 30:5 - Swahili Revised Union Version Naye Bilha akapata mimba, akamzalia Yakobo mwana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Bilha akapata mimba na kumzalia Yakobo mtoto wa kiume. Biblia Habari Njema - BHND Bilha akapata mimba na kumzalia Yakobo mtoto wa kiume. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Bilha akapata mimba na kumzalia Yakobo mtoto wa kiume. Neno: Bibilia Takatifu naye Bilha akapata mimba, akamzalia Yakobo mwana. Neno: Maandiko Matakatifu Bilha akapata mimba, naye akamzalia Yakobo mwana. BIBLIA KISWAHILI Naye Bilha akapata mimba, akamzalia Yakobo mwana. |
Raheli akasema, Mungu amenipa haki yangu, naye amesikia sauti yangu, akanipa mwana. Kwa hiyo akamwita jina lake Dani.
Ikawa Israeli alipokuwa akikaa katika nchi ile, Reubeni akaenda akalala na Bilha, suria wa babaye; Israeli akasikia habari. Basi hao wana wa Yakobo walikuwa kumi na wawili.
Hao ndio wana wa Bilha, ambaye Labani alimpa Raheli, binti yake, naye akamzalia Yakobo hao; wote walikuwa watu saba.
Hawa ndio wana wa Israeli; Reubeni, na Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Zabuloni;
Katika wana wa Dani, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani;
Akampa agano la tohara; basi Abrahamu akamzaa Isaka, akamtahiri siku ya nane. Isaka akamzaa Yakobo. Yakobo akawazaa wale kumi na wawili, wazee wetu.