Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Matendo 7:8 - Swahili Revised Union Version

8 Akampa agano la tohara; basi Abrahamu akamzaa Isaka, akamtahiri siku ya nane. Isaka akamzaa Yakobo. Yakobo akawazaa wale kumi na wawili, wazee wetu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Halafu Mungu akafanya naye agano ambalo tohara ni ishara yake. Hivyo, Abrahamu alimtahiri mtoto wake Isaka siku ya nane baada ya kuzaliwa. Na Isaka, vivyo hivyo, alimtahiri Yakobo. Naye Yakobo aliwatendea wale mababu kumi na wawili vivyo hivyo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Halafu Mungu akafanya naye agano ambalo tohara ni ishara yake. Hivyo, Abrahamu alimtahiri mtoto wake Isaka siku ya nane baada ya kuzaliwa. Na Isaka, vivyo hivyo, alimtahiri Yakobo. Naye Yakobo aliwatendea wale mababu kumi na wawili vivyo hivyo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Ndipo akampa Ibrahimu agano la tohara. Naye Ibrahimu akamzaa Isaka na kumtahiri siku ya nane. Baadaye Isaka akamzaa Yakobo, naye Yakobo akawazaa wale baba zetu wa zamani kumi na wawili.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Ndipo akampa Ibrahimu Agano la tohara. Naye Ibrahimu akamzaa Isaka na kumtahiri siku ya nane. Baadaye Isaka akamzaa Yakobo, naye Yakobo akawazaa wale wazee wetu kumi na wawili.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

8 Akampa agano la tohara; basi Abrahamu akamzaa Isaka, akamtahiri siku ya nane. Isaka akamzaa Yakobo. Yakobo akawazaa wale kumi na wawili, wazee wetu.

Tazama sura Nakili

Matendo 7:8
20 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA akaona ya kwamba Lea hakupendwa, naye akafungua tumbo lake; bali Raheli alikuwa hazai.

Naye Bilha akapata mimba, akamzalia Yakobo mwana.

Wakasafiri kutoka Betheli, na kabla ya kufika Efrata, Raheli akashikwa na uchungu wa kuzaa, na uchungu wake ulikuwa mkali.

Ikawa hapo katika kutoa roho yake, maana alikufa, akamwita jina lake Benoni, lakini babaye alimwita Benyamini.

Na Abrahamu naye akamzaa Isaka. Wana wa Isaka; Esau, na Israeli.

Abrahamu alimzaa Isaka; Isaka akamzaa Yakobo; Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake;

Musa aliwapa tohara; lakini si kwamba yatoka kwa Musa, bali kwa mababa; nanyi mwatahiri mtu siku ya sabato.

Wanaume, ndugu zangu, mniwie radhi, niseme kwa ujasiri mbele yenu habari za baba yetu mkuu, Daudi, ya kuwa alifariki akazikwa, na kaburi lake liko kwetu hata leo.

Alihesabiwaje basi? Alipokwisha kutahiriwa, au kabla hajatahiriwa? Si baada ya kutahiriwa, bali kabla ya kutahiriwa.

Ndugu zangu, nanena kwa jinsi ya kibinadamu. Lijapokuwa ni agano la mwanadamu, hata hivyo likiisha kuthibitika, hakuna mtu alibatilishaye, wala kuliongeza neno.

Nisemalo ni hili; agano lililothibitishwa kwanza na Mungu, torati iliyotokea miaka mia nne na thelathini baadaye hailitangui, hata kuibatilisha ile ahadi.

Basi, angalieni jinsi mtu huyo alivyokuwa mkuu, ambaye Abrahamu, baba yetu mkuu, alimpa sehemu ya kumi ya nyara.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo