Isaka akawa mwenye miaka arubaini alipomtwaa Rebeka binti Bethueli, Mshami, wa Padan-aramu, ndugu wa Labani, Mshami, kuwa mke wake.
Mwanzo 28:7 - Swahili Revised Union Version na ya kuwa Yakobo amewatii babaye na mamaye, akaenda Padan-aramu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alitambua pia kuwa Yakobo alimtii mama yake na baba yake, akaenda Padan-aramu. Biblia Habari Njema - BHND Alitambua pia kuwa Yakobo alimtii mama yake na baba yake, akaenda Padan-aramu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alitambua pia kuwa Yakobo alimtii mama yake na baba yake, akaenda Padan-aramu. Neno: Bibilia Takatifu tena kwamba Yakobo amewatii baba yake na mama yake, naye ameenda Padan-Aramu. Neno: Maandiko Matakatifu tena kwamba Yakobo amewatii baba yake na mama yake naye amekwenda Padan-Aramu. BIBLIA KISWAHILI na ya kuwa Yakobo amewatii babaye na mamaye, akaenda Padan-aramu. |
Isaka akawa mwenye miaka arubaini alipomtwaa Rebeka binti Bethueli, Mshami, wa Padan-aramu, ndugu wa Labani, Mshami, kuwa mke wake.
Na sasa, mwanangu, sikia sauti yangu, uondoke, ukimbilie kwa Labani, ndugu yangu huko Harani;
Esau akaona ya kwamba Isaka amembariki Yakobo na kumtuma Padan-aramu, ili ajitwalie mke huko, na katika kumbariki akamwagiza, akasema, Usioe mke wa binti za Kanaani,
Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
Jicho la mtu amdhihakiye babaye, Na kudharau kumtii mamaye; Kunguru wa bondeni wataling'oa, Na vifaranga vya tai watalila.
Kila mtu na amche mama yake, na baba yake, nanyi mtazitunza Sabato zangu; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza katika Bwana.