Ndipo Abrahamu akaanguka kifudifudi akacheka, akasema moyoni, Je! Mtu wa umri wa miaka mia moja, kwake atazaliwa mtoto? Naye Sara mwenye umri wa miaka tisini atazaa?
Mwanzo 23:1 - Swahili Revised Union Version Basi umri wake Sara ulikuwa miaka mia moja na ishirini na saba, ndio umri wake Sara. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sara aliishi miaka 127. Hiyo ndiyo iliyokuwa miaka ya maisha yake Sara. Biblia Habari Njema - BHND Sara aliishi miaka 127. Hiyo ndiyo iliyokuwa miaka ya maisha yake Sara. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sara aliishi miaka 127. Hiyo ndiyo iliyokuwa miaka ya maisha yake Sara. Neno: Bibilia Takatifu Sara aliishi miaka mia moja na ishirini na saba (127). Neno: Maandiko Matakatifu Sara aliishi akawa na umri wa miaka mia na ishirini na saba. BIBLIA KISWAHILI Basi umri wake Sara ulikuwa miaka mia moja na ishirini na saba, ndio umri wake Sara. |
Ndipo Abrahamu akaanguka kifudifudi akacheka, akasema moyoni, Je! Mtu wa umri wa miaka mia moja, kwake atazaliwa mtoto? Naye Sara mwenye umri wa miaka tisini atazaa?
Sara akafa katika Kiriath-arba, ndio Hebroni, katika nchi ya Kanaani. Abrahamu akamlilia na kumwombolezea Sara.
Isaka akamwingiza Rebeka katika hema ya mama yake, Sara, akamtwaa Rebeka, akawa mkewe, akampenda; Isaka akafarijika kwa ajili ya kufa kwa mama yake.