Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 24:67 - Swahili Revised Union Version

67 Isaka akamwingiza Rebeka katika hema ya mama yake, Sara, akamtwaa Rebeka, akawa mkewe, akampenda; Isaka akafarijika kwa ajili ya kufa kwa mama yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

67 Basi, Isaka akamchukua Rebeka ndani ya hema iliyokuwa ya Sara mama yake, akawa mke wake. Isaka akampenda Rebeka na kupata faraja baada ya kifo cha mama yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

67 Basi, Isaka akamchukua Rebeka ndani ya hema iliyokuwa ya Sara mama yake, akawa mke wake. Isaka akampenda Rebeka na kupata faraja baada ya kifo cha mama yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

67 Basi, Isaka akamchukua Rebeka ndani ya hema iliyokuwa ya Sara mama yake, akawa mke wake. Isaka akampenda Rebeka na kupata faraja baada ya kifo cha mama yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

67 Isaka akamwingiza Rebeka katika hema la Sara mama yake. Isaka akamchukua Rebeka, hivyo akawa mke wake. Isaka akampenda; akafarijika baada ya kifo cha mama yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

67 Ndipo Isaka akamwingiza Rebeka katika hema la Sara mama yake, Isaka akamchukua Rebeka, hivyo akawa mke wake. Isaka akampenda, akafarijika baada ya kifo cha mama yake.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 24:67
16 Marejeleo ya Msalaba  

Basi Abrahamu akaenda hima hemani kwa Sara, akasema, Tayarisha haraka vipimo vitatu vya unga safi, uukande, ufanye mikate.


Yule mtumishi akamwambia Isaka mambo yote aliyoyatenda.


Abrahamu alioa mke mwingine jina lake akiitwa Ketura.


Isaka akawa mwenye miaka arubaini alipomtwaa Rebeka binti Bethueli, Mshami, wa Padan-aramu, ndugu wa Labani, Mshami, kuwa mke wake.


Yakobo akampenda Raheli akasema, Nitakutumikia miaka saba kwa kumpata Raheli, binti yako mdogo.


Wanawe wote, na binti zake wote, wakaondoka wamtulize, lakini akakataa kutulizwa, akasema, La! Nitashuka kaburini kwa mwanangu, nikiomboleza. Basi baba yake akamlilia.


Siku nyingi zikapita, akafa binti Shua, mkewe Yuda. Yuda akafarijika, akaenda kwa watu wake wawakatao kondoo manyoya huko Timna, yeye na mwenzake Hira, Mwadulami.


Ningekuongoza nyumbani mwa mamangu, Naye angenifundisha; Ningekunywesha divai iliyokolea, Divai mpya ya mkomamanga wangu.


Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.


Kwa kuwa tunawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo