Basi Abimeleki akatwaa kondoo, na ng'ombe, na watumwa, na wajakazi, akampa Abrahamu, akamrudishia Sara mkewe.
Mwanzo 21:22 - Swahili Revised Union Version Ikawa wakati ule Abimeleki, na Fikoli mkuu wa jeshi lake, wakamwambia Abrahamu, wakinena, Mungu yu pamoja nawe katika yote unayotenda. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakati huo, Abimeleki pamoja na Fikoli, mkuu wa jeshi lake, alimwendea Abrahamu, akamwambia, “Mungu yuko pamoja nawe katika kila kitu unachofanya. Biblia Habari Njema - BHND Wakati huo, Abimeleki pamoja na Fikoli, mkuu wa jeshi lake, alimwendea Abrahamu, akamwambia, “Mungu yuko pamoja nawe katika kila kitu unachofanya. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakati huo, Abimeleki pamoja na Fikoli, mkuu wa jeshi lake, alimwendea Abrahamu, akamwambia, “Mungu yuko pamoja nawe katika kila kitu unachofanya. Neno: Bibilia Takatifu Wakati huo Abimeleki na Fikoli mkuu wa majeshi yake wakamwambia Ibrahimu, “Mungu yu pamoja nawe katika kila kitu unachofanya. Neno: Maandiko Matakatifu Wakati huo Abimeleki na Fikoli mkuu wa majeshi yake wakamwambia Ibrahimu, “Mungu yu pamoja nawe katika kila kitu unachofanya. BIBLIA KISWAHILI Ikawa wakati ule Abimeleki, na Fikoli mkuu wa jeshi lake, wakamwambia Abrahamu, wakinena, Mungu yu pamoja nawe katika yote unayotenda. |
Basi Abimeleki akatwaa kondoo, na ng'ombe, na watumwa, na wajakazi, akampa Abrahamu, akamrudishia Sara mkewe.
Abrahamu akamwomba Mungu, Mungu akamponya Abimeleki, na mkewe, na wajakazi wake, nao wakazaa wana.
Abrahamu akanena juu ya Sara mkewe, “Huyu ni dada yangu”. Basi Abimeleki mfalme wa Gerari akatuma watu wakamtwaa Sara.
Ndipo Abimeleki akamwendea kutoka Gerari, pamoja na Ahuzathi rafiki yake, na Fikoli, jemadari wa jeshi lake.
Wakasema, Hakika tuliona ya kwamba BWANA alikuwa pamoja nawe; nasi tukasema, Na tuapiane, sisi na wewe, na kufanya mapatano nawe
Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia.
Labani akamwambia, Iwapo nimeona fadhili machoni pako, kaa, maana nimetambua ya kwamba BWANA amenibariki kwa ajili yako.
Naona uso wa baba yenu, kwamba hanitazami vema kama hapo awali. Lakini Mungu wa baba yangu amekuwa pamoja nami.
wakaja ngomeni kwa Tiro, na kwa miji yote ya Wahivi, na ya Wakanaani; tena wakaenda katika Negebu ya Yuda huko Beer-sheba.
Basi Sulemani, mwana wa Daudi, alijiimarisha katika ufalme wake, naye BWANA, Mungu wake, alikuwa pamoja naye, akamtukuza mno.
BWANA asema hivi, Kazi ya Misri, na bidhaa ya Kushi, na Waseba, watu walio warefu, watakujia, nao watakuwa wako; watakufuata; watakuja katika minyororo; wataanguka chini mbele yako, watakuomba, wakisema, Hakika Mungu yu ndani yako; wala hapana mwingine, hapana Mungu tena.
Fanyeni shauri pamoja, nalo litabatilika; Semeni neno, lakini halitasimama; Kwa maana Mungu yu pamoja nasi.
BWANA wa majeshi asema hivi, Siku hizo watu kumi, wa lugha zote za mataifa, wataushika upindo wa nguo yake yeye aliye Myahudi; naam, wataushika wakisema, Tutakwenda pamoja nanyi, kwa maana tumesikia kwamba Mungu yuko pamoja nanyi.
Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.
siri za moyo wake huwa wazi; na hivyo atamwabudu Mungu, akianguka kifudifudi, na kukiri ya kuwa Mungu yuko kati yenu bila shaka.
Msiwe na tabia ya kupenda fedha; muwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kamwe, wala sitakuacha.
BWANA akamwambia Yoshua, Hivi leo nitaanza kukutukuza mbele ya Israeli wote, wapate kujua ya kuwa mimi nitakuwa pamoja na wewe, kama nilivyokuwa pamoja na Musa.
Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda.
Naye Daudi akamwapia Sauli. Kisha Sauli akaenda zake kwao; lakini Daudi na watu wake wakapanda kwenda ngomeni.
Samweli akakua, naye BWANA alikuwa pamoja naye, wala hakuliacha neno lake lolote lianguke chini.