nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;
Mwanzo 17:2 - Swahili Revised Union Version Nami nitafanya agano langu nawe, nami nitakuzidishia sana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nami nitafanya agano nawe na kuwazidisha wazawa wako.” Biblia Habari Njema - BHND Nami nitafanya agano nawe na kuwazidisha wazawa wako.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nami nitafanya agano nawe na kuwazidisha wazawa wako.” Neno: Bibilia Takatifu Nitafanya agano kati yangu na wewe, nami nitakuzidisha sana.” Neno: Maandiko Matakatifu Nami nitafanya Agano langu kati yangu na wewe, nami nitakuzidisha sana sana.” BIBLIA KISWAHILI Nami nitafanya agano langu nawe, nami nitakuzidishia sana. |
nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;
Na uzao wako nitaufanya uwe kama mavumbi ya nchi; ikiwa mtu ataweza kuyahesabu mavumbi ya nchi, uzao wako nao utahesabika.
Siku ile BWANA akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,
Akamtoa nje, akasema, Tazama juu mbinguni kisha uzihesabu nyota, kama unaweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.
katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki lango la adui zao;
Lakini BWANA akawahurumia, akawasikitikia, na kuwaangalia, kwa ajili ya agano lake na Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, wala hakutaka kuwaangamiza, wala hakuwatupa usoni pake bado.
ambao ni Waisraeli, wenye kule kufanywa wana, na ule utukufu, na maagano, na kupewa torati, na ibada ya Mungu, na ahadi zake;