Kwa hao nchi za pwani za mataifa ziligawanyikana kuwa nchi zao, kila moja kwa lugha yake, kwa jamaa zao, kufuata mataifa yao.
Mwanzo 10:6 - Swahili Revised Union Version Na wana wa Hamu ni Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watoto wa kiume wa Hamu walikuwa Kushi, Misri, Puti na Kanaani. Biblia Habari Njema - BHND Watoto wa kiume wa Hamu walikuwa Kushi, Misri, Puti na Kanaani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watoto wa kiume wa Hamu walikuwa Kushi, Misri, Puti na Kanaani. Neno: Bibilia Takatifu Wana wa Hamu walikuwa: Kushi, Misri, Putu na Kanaani. Neno: Maandiko Matakatifu Wana wa Hamu walikuwa: Kushi, Misraimu, Putu na Kanaani. BIBLIA KISWAHILI Na wana wa Hamu ni Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani. |
Kwa hao nchi za pwani za mataifa ziligawanyikana kuwa nchi zao, kila moja kwa lugha yake, kwa jamaa zao, kufuata mataifa yao.
Wana wa Nuhu waliotoka katika safina, ni Shemu, na Hamu, na Yafethi; na Hamu ndiye baba wa Kanaani.
Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.
Wakaona malisho ya unono, mazuri, na nchi yenyewe ilikuwa wazi, tulivu na yenye amani; kwani waliokaa huko zamani walikuwa watu wa Hamu.
Na itakuwa katika siku hiyo, Bwana atapeleka mkono wake mara ya pili, ili ajipatie watu wake watakaosalia, kutoka Ashuru, na kutoka Misri, na kutoka Pathrosi, na kutoka Kushi, na kutoka Elamu, na kutoka Shinari, na kutoka Hamathi, na kutoka visiwa vya bahari.
Haya! Pandeni, enyi farasi; Jihimizeni, enyi magari ya vita; Mashujaa nao na watoke nje Kushi na Puti, watumiao ngao; Nao Waludi, washikao uta na kuupinda.
Watu wa Uajemi na Ludi na Putu walikuwa katika jeshi lako, watu wako wa vita; walitungika ngao na chapeo ndani yako; wakadhihirisha uzuri wako.