Akasema, Na atukuzwe BWANA, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, ambaye hakuacha rehema zake na kweli yake kwa bwana wangu. BWANA akaniongoza mimi nami njiani hata nyumba ya nduguze bwana wangu.
Mika 7:20 - Swahili Revised Union Version Wewe utamtimilizia Yakobo kweli yako, na Abrahamu rehema zako, ulizowaapia baba zetu tangu siku za kale. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Utaonesha uaminifu wako na rehema zako kwa wazawa wa Abrahamu na wa Yakobo, kama ulivyowaahidi wazee wetu tangu zamani. Biblia Habari Njema - BHND Utaonesha uaminifu wako na rehema zako kwa wazawa wa Abrahamu na wa Yakobo, kama ulivyowaahidi wazee wetu tangu zamani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Utaonesha uaminifu wako na rehema zako kwa wazawa wa Abrahamu na wa Yakobo, kama ulivyowaahidi wazee wetu tangu zamani. Neno: Bibilia Takatifu Utakuwa wa kweli kwa Yakobo, nawe utamwonesha Ibrahimu rehema, kama ulivyowaahidi kwa kiapo baba zetu siku za kale. Neno: Maandiko Matakatifu Utakuwa wa kweli kwa Yakobo, nawe utamwonyesha Ibrahimu rehema, kama ulivyowaahidi kwa kiapo baba zetu siku za kale. BIBLIA KISWAHILI Wewe utamtimilizia Yakobo kweli yako, na Abrahamu rehema zako, ulizowaapia baba zetu tangu siku za kale. |
Akasema, Na atukuzwe BWANA, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, ambaye hakuacha rehema zake na kweli yake kwa bwana wangu. BWANA akaniongoza mimi nami njiani hata nyumba ya nduguze bwana wangu.
mimi sistahili hata kidogo hizo rehema zote na kweli yote uliyomfanyia mtumwa wako; maana nilivuka mto huo wa Yordani na fimbo yangu tu, na sasa nimekuwa makundi mawili.
Tazama, nitauletea afya na kupona, nami nitawaponya; nami nitawafunulia wingi wa amani na kweli.
Na itakuwa, kwa sababu mnazisikiliza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi BWANA, Mungu wako, atakutimilizia agano na rehema aliyowaapia baba zako;
bali kwa sababu BWANA anawapenda, na kwa sababu alitaka kukitimiza kiapo chake alichowaapia baba zenu, ndiyo sababu BWANA akawatoa kwa mkono wa nguvu, akawakomboa katika nyumba ya utumwa, katika mkono wa Farao, mfalme wa Misri.